Sport
Dollar
43,1626
0.11 %Euro
50,3395
0 %Gram Gold
6.388,0600
0.32 %Quarter Gold
10.530,2200
0.26 %Silver
120,6000
2.14 %Mamlaka hapo awali zilisema baadhi ya vito vilivyoibiwa tayari vimesafirishwa kwa njia ya magendo na kuvuka mipaka ya nchi hiyo, na sehemu kubwa ya vito hivyo bado haijulikani ilipo.
Sudan imeandaa sherehe maalum siku ya Jumanne, Januari 13, huko Port Sudan baada ya kutangaza kurudishwa kwa vito vya kale 570 vyenye thamani vilivyoibiwa wakati wa mgogoro unaoendelea nchini humo.
Katika mwaliko rasmi, Waziri wa Utamaduni, Habari na Utalii Khalid Al-Eisir alitangaza kuwa serikali itafungua rasmi vito vilivyorejeshwa, ambavyo vinaonesha nyakati tofauti za kihistoria, kuanzia zama za historia ya kale hadi enzi za kisasa.
Waziri Al-Eisir alielezea kurudishwa kwa vito hivyo vya kale kama sehemu ya mafanikio makubwa ya kitaifa, huku akisema hatua hiyo inaonyesha azma ya serikali ya kulinda urithi na ustaarabu wa Sudan na kudai tena mali yake ya kitamaduni, ripoti za vyombo vya habari vya serikali SUNA zinaonyesha.
Makumbusho ya Sudan yaliathirika kwa kiasi kikubwa na wizi uliofanyika katika siku za awali za mapigano kati ya jeshi la Sudan na Jeshi la RSF vilivyoanza Aprili 2023. Maelfu ya vito vyenye thamani kubwa, vingi vyao kutoka Ufalme wa Kush wa takriban miaka 3,000 iliyopita, vilitoweka.
Vito vilivyoibiwa
Kwa mujibu wa maafisa, vito kutoka makumbusho zaidi ya 20 nchini kote viliibiwa au kuharibiwa, na hasara inakadiriwa kufikia takriban dola za Kimarekani milioni 110.
Maeneo yaliyolengwa wakati wa mapigano yalikuw Makumbusho ya Ikulu ya Rais, Makumbusho ya Vikosi vya Ulinzi, Makumbusho ya Nyumba ya Khalifa, Makumbusho ya Etnografia, na Makumbusho ya Historia ya Asili katika Chuo Kikuu cha Khartoum.
Awali, Mamlaka zilisema kuwa baadhi ya vitu vilivyochukuliwa tayari vilivushwa kwa njia za magendo katika mipaka ya nchi hiyo na sehemu kubwa ya vito hivyo bado haijulikani ilipo.
Hata hivyo, tangu Aprili 2025, serikali ya Sudan imekuwa ikishirikiana na Interpol na UNESCO kurejesha mali za kitamaduni zilizoibiwa.
Septemba mwaka uliopita, UNESCO ilitoa tahadhari ya kimataifa ikionya nyumba za makumbusho, wakusanyaji, na nyumba za mnada kutochukua au kuuza mali za kitamaduni zinazotoka Sudan.
Comments
No comments Yet
Comment