Dollar

43,1655

0.08 %

Euro

50,4542

0.1 %

Gram Gold

6.379,0800

0.18 %

Quarter Gold

10.502,7600

0 %

Silver

118,1400

0.05 %

IShowSpeed, anayejulikana pia kama Speed, ni nyota maarufu wa mitandao ya kijamii kutoka Marekani ambaye hivi karibuni amevutia hisia za maelfu ya vijana barani Afrika, hasa Kenya.

IShowSpeed ni nani, nyota wa mtandaoni aliyevuma Kenya?

Akiwa na umri wa miaka 2, amezuru nchi karibia nane katika bara la Afrika, ziara iliyoanza Desemba 29, 2025.

Baadhi ya nchi alizotembelea ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Eswatini, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na hatimaye Kenya. Ziara yake ya Kenya, iliyofanyika Jumapili, Januari 11, ilikuwa ya kipekee na ya kihistoria.

Rais wa Kenya, William Ruto, alimkaribisha rasmi kupitia video iliyosambaa sana kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok, akisema: "Jambo, IShowSpeed. Karibu Kenya. Kenya si nchi nyingine tu, Kenya ni moyo, ni hisia, Kenya ni nyumbani."

Akiwa Nairobi, IShowSpeed alionyesha mubashara (livestream) matembezi yake katikati ya jiji huku akifuatwa na makumi ya vijana.

Katika ziara yake alitembelea hifadhi ya taifa ya Nairobi, soko kubwa la jiji, kuzunguka mji kutumia helikopta, na kushuhudia kwa karibu utamaduni wa usafiri wa umma wa Kenya. Safari hiyo ilionesha kwa uwazi uchangamfu na nishati ya nchi.

Kupitia chaneli yake ya YouTube akiwa Kenya, IShowSpeed alipata wafuasi wapya zaidi ya 360,000, jambo lililomfanya kupata idadi ya wafuasi milioni 48 kwenye YouTube. Wakati huohuo, zaidi ya watu 200,000 walikuwa wakifuatilia mubashara chaneli yake alipokuwa katika ziara hiyo.

Akitoa shukrani zake kwa Wakenya, alisema: "Nawapenda sana nyote. Kenya, hatutoisahau kamwe."

Lakini IShowSpeed ni nani hasa?

Jina lake halisi ni Darren Jason Watkins Junior, alizaliwa Januari 21, 2005, katika jimbo la Ohio, Marekani. Alikulia huko na ndugu wawili. Alianza kutengeneza maudhui kwenye YouTube mwaka 2016 alipokuwa bado kijana mdogo, akijikita zaidi kwenye michezo ya video kama FIFA na NBA.

Wakati wa janga la COVID-19, aliongeza kasi ya matangazo yake ya mubashara ya michezo ya video, huku pia akishirikisha sehemeu ya maisha yake binafsi. Mwaka 2023, mwaka huohuo aliomaliza shule ya upili, alianza kusafiri duniani.

Nishati yake ya kipekee, uwezo wa kimichezo na vitendo vyake visivyotabirika mara nyingi vinaendana na jina lake la kisanii, “I Show Speed.”

Ameeleza kuwa alichagua jina hilo alipokuwa na umri wa miaka 12 kwa akaunti yake ya PlayStation Network. Wakati wa michezo yake, huonesha hisia kali, ikiwa ni pamoja na hasira au furaha kupita kiasi.

Zaidi ya michezo ya video, chaneli yake ya YouTube huonesha tamaduni, lugha na desturi za mataifa mbalimbali anayoyatembelea. Septemba 2024, alipata watazamaji zaidi ya milioni moja waliokuwa wakifuatilia mubashara chaneli yake alipokuwa katika ziara yake nchini Indonesia.

Kwa sasa, IShowSpeed ana zaidi ya wafuasi milioni 48 kwenye YouTube, milioni 46 kwenye TikTok, milioni 44 kwenye Instagram, na zaidi ya milioni 6 kwenye Facebook na Snapchat, na karibu milioni 4 kwenye mtandao wa X. Kwa jumla, ana zaidi ya wafuasi milioni 150 kwenye majukwaa yake makuu sita ya mitandao ya kijamii duniani.

Kwa kifupi, IShowSpeed si tu mchezaji wa michezo ya video (video games), bali ni nyota wa kimataifa anayewaunganisha vijana duniani kupitia burudani, utamaduni na nishati isiyo kifani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#