Sport
Dollar
43,1673
0.12 %Euro
50,3994
0.13 %Gram Gold
6.364,7800
-0.04 %Quarter Gold
10.488,6100
-0.13 %Silver
118,9200
0.71 %Serikali ya Sudani Jumatatu ilipitia mipango ya kujenga upya mji mkuu wa Khartoum na kurudisha huduma za msingi, baada ya serikali kuchukua uamuzi wa kuendelea na shughuli zake kutoka mjini humo.
Serikali ya Sudan Jumatatu ilipitia upya mipango yake ya kuijuenga Khartoum na kurudisha huduma muhimu, hii ni kufuatia uamuzi wa serikali wa kurudisha shughuli zake katika mji huo baada ya zaidi ya miaka miwili.
Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa mkutano uliofanyika Khartoum kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Mpito Abdel Fattah al-Burhan na Waziri Mkuu Kamel Idris, siku moja baada ya serikali kutangaza kutudi katika mji mkuu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mapigano na vikosi vya RSF mwezi Aprili 2023.
Wakati wote wa mapigano, serikali imekuwa ikifanya shughuli zake katika mji wa Port Sudan, uliopo katika pwani ya Bahari Nyekundu, baada ya uharibifu mkubwa kufanyika Khartoum na idadi kubwa ya wakazi wake kukimbia makazi yao.
Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema mkutano huo umejikita zaidi katika kuchukua hatua za kujenga upya miundombinu na kufufua huduma muhimu ili kujenga mazingira ya watu kurudi katika makazi yao.
Hatua mpya
Burhan na Idris pia wamejadili mkakati mpana zaidi wa kuandaa mji mkuu kwa kufunguliwa kwa taasisi za serikali kuu, huku wakisisitiza umuhimu wa jitihada shirikishi kati ya mamlaka na jamii ili kukabiliana na changamoto zilizopo na kurahisisha ujenzi.
Mazungumzo hayo yalifuatia tangazo la jeshi la Sudan la mwezi Mei la kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Khartoum na kuvitimua vikosi vya RSF katika eneo hilo.
Mwenzi Julai, kuliundwa kamati iliyojikita kusimamia maandalizi ya wananchi kurudi na taasisi za serikali kuanza kutoa huduma.
Kwa mujibu wa taarifa, mkutano huo unaashiria hatua mpya ambayo serikali kwamba serikali kwa mara nyengine inasimamia shughuli za serikali kutoka mji mkuu, katika hali ambayo inayoelezea kuimarisha kwa hali ya usalama.
Madhara ya vita
Katika majibu 18 ya Sudan, RSF inadhibiti majimbo 5 ya jimbo la Darfur upande wa magharibi, isipokuwa baadhi ya maeneo ya kaskazini ya Kaskazini mwa Darfur ambayo bado yako chini ya udhibiti wa jeshi.
Kwa upande wake, jeshi, linadhibiti sehemu kubwa ya majimbo 13 yaliyobaki ya kusini, kaskazini, mashariki, na kati, ikiwemo mji mkuu wa Khartoum.
Mgogoro kati ya jeshi la Sudan na RSF, ambao umeanza Aprili 2023, umeaua maelfu ya watu na mamilioni kukosa makazi.
Comments
No comments Yet
Comment