Sport
Dollar
38,8442
0.26 %Euro
43,5099
-0.06 %Gram Gold
4.040,8300
0.18 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imetoa taarifa ikisema kuwa "inakanusha na kukataa kabisa taarifa za kupotosha na uchochezi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii".
Siku ya Alhamisi serikali ya Sudan Kusini imekanusha kuwa Rais Salva Kiir amefariki dunia, kufuatia uvumi katika mitandao ya kijamii.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 73 na ambaye amekuwepo madarakani kwa muda mrefu amekuwa akizushiwa kuwa anaumwa sana katika siku za hivi karibuni.
Lakini ameonekana kwenye picha katika miezi ya karibu akikutana na viongozi mbalimbali na kuagiza mabadiliko kadhaa ndani ya serikali.
Pia amechukua hatua kali dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu na makamu wa rais wa kwanza wa nchi hiyo, Riek Machar, na kuagiza asiruhusiwe kutoka nje ya nyumba yake pamoja na kuwakamata washirika wake kadhaa.
‘Uzushi usio na msingi’
Jumatano jioni, taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa Kiir, kwa maneno ya mtu mmoja maarufu nchini Kenya, "amefariki dunia".
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini ikatoa taarifa siku iliyofuata, ikisema "inakanusha na kukataa kabisa taarifa za kupotosha na uchochezi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Mheshimiwa Rais Salva Kiir Mayardit amefariki".
Taarifa hizo kwenye mitandao "zilikuwa hazina msingi na zenye uchochezi ambazo zimetengenezwa na maadui wa amani, maendeleo, na ujenzi wa taifa na uthabiti", iliongeza.
Inajiri huku Sudan Kusini ikikabiliwa na hali nyingine ya ukosefu wa usalama, na kukiwa na makabiliano kati ya vikosi vinavyomuunga mkono Kiir na vile vya Machar katika maeneo mbalimbali ya nchi, kusababisha hofu ya kuanza tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Comments
No comments Yet
Comment