Dollar

38,8506

0.32 %

Euro

43,5622

0.08 %

Gram Gold

4.037,6900

0.1 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kuridhishwa kwake na kusitishwa kwa mapigano nchini Libya baada ya vita kuzuka kati ya makundi yenye silaha maeneo ya mji mkuu wa Tripoli.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa mazungumzo Libya baada ya kusitishwa mapigano mji mkuu

Siku ya Alhamisi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kuridhishwa kwake na kusitishwa kwa mapigano nchini Libya baada ya vita kuzuka kati ya makundi yenye silaha katika maeneo ya mji wa Tripoli.

"Katibu Mkuu amefuatilia kwa makini makubaliano ya kusitishwa mapigano yaliyofikiwa mjini Tripoli jana na kutoa wito kwa pande zote kuchukua hatua za kuendeleza hilo na kuwa na utulivu zaidi kupitia majadiliano," msemaji Farhan Haq amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kushtushwa kwake na "kuongezeka kwa haraka" kwa mapigano katika mji mkuu, na kusema: "Kuongezeka huku kumesababiosha makundi yenye silaha kutoka nje ya mji na kushambulia vikali mitaa ya mji huo, ni hali ya kushtusha."

Guterres alitoa salamu zake za rambirambi kwa raia waliouawa wasiopungua wanane katika mapigano ya hivi karibuni mjini Tripoli.

'Majadiliano kwa nia njema'

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwalinda raia, Guterres ametoa wito kwa pande zote ‘‘kujadiliana kwa dhati na nia njema ili kutatua chimbuko la mapigano hayo."

Taarifa hiyo imeeleza msimamo wa Umoja wa Mataifa kuhusu juhudi za mchakato wa amani, na kusema: "Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa ofisi zake kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa makubaliano ambayo yataleta amani ya kudumu na utulivu nchini Libya."

Wizara ya ulinzi ya Libya imesema siku ya Jumatano kuwa kusitishwa kwa mapigano kulifanyika baada ya kuzuka kwa makabiliano mapya ya makundi yenye silaha.

Taarifa ilisema walisitisha mapigano katika maeneo yote ya mjini Tripoli ambayo yalikuwa yanakabiliwa na vurugu kama sehemu ya juhudi hizo ili "kulinda raia, na taasisi za taifa, pamoja na kuepusha kuongezeka kwa vita."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#