Dollar

38,7052

-0.17 %

Euro

43,5349

0.29 %

Gram Gold

3.999,6200

0.97 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rigathi Gachagua amesema kuwa chama cha DCP kitatanguliza sauti za Wakenya, hivyo basi kauli mbiu ya chama "Skiza Wakenya" ambayo inamaanisha "Sikiliza Wakenya"

Naibu rais wa zamani Kenya aanzisha chama chake

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amezindua rasmi chama chake cha kisiasa kinachoitwa Democracy for the Citizens Party (DCP) yani Chama cha Demokrasia ya Wananchi.

Gachagua aliondolewa kwa nguvu katika wadhifa wake wa makamu wa rais na Bunge la nchi hiyo Oktoba 2024.

Katika hafla iliyofanyika Alhamisi jijini Nairobi, Mei 15, Gachagua alizindua chama hicho atakachokitumia kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2027.

Gachagua alisema kuwa amekaa kwa muda wa miezi 6 iliyopita nyumbani kwake kufanya mashauriano ya kusaidia kuunda chama chake cha kisiasa.

Alibainisha kuwa DCP kimeundwa katika msingi wa kutoa uongozi bora kwa Wakenya na kuwaondoa katika matatizo ya muda mrefu ya uongozi mbaya.

"Wakenya wametuambia kwa ujasiri kwamba wana suluhu ya matatizo yanayowakabili. Wakenya wametuomba tuanzishe chama ambacho kitaunda serikali ya wananchi kwa ajili ya wananchi," Gahagua alisema wakati wa uzinduzi wa chama hicho.

Uongozi wa chama cha Gachagua

Chama hicho kitaongozwa na Rigathi Gachagua, huku aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala akiwa Naibu Kiongozi wa Chama.

Malala alifukuzwa kama Katibu Mkuu wa chama tawala cha Rais William Ruto, UDA Disemba 2023.

Aliyekuwa Seneta wa Meru na Waziri wa Kilimo Mithika Linturi atakuwa Katibu Mkuu wa Kitaifa. Linturi alifutwa kazi na Rais William Ruto mwaka jana baada ya maandamano ya vijana maarufu kama Gen Z.

Akiwa waziri alijipata katika kashfa ya wizra ya kilimo kuwapa Wakenya mbolea iliyokuwa chini ya kiwango.

Gachagua amesema kuwa chama cha DCP hakina wagombeaji wanaopendelewa na kitatanguliza sauti za Wakenya, hivyo basi kauli mbiu ya chama "Skiza Wakenya" ambayo inamaanisha "Sikiliza Wakenya."

Amesema kuwa chama hicho kinapenda ushirikishwaji na kimejumuisha wawakilishi kutoka makundi yote nchini kote, ikiwa ni pamoja na vijana maarufu kama Gen Z.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#