Dollar

38,8657

0.28 %

Euro

43,5418

-0.05 %

Gram Gold

4.044,0200

0.26 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema kuwa mashambulizi kwa vituo vya afya yanaongezeka nchini Sudan Kusini.

Mfumo wa afya wa Sudan Kusini 'unasambaratika': Madaktari Wasio na Mipaka

Siku ya Alhamisi Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lilisema kuwa mashambulizi dhidi ya vituo vya afya nchini Sudan Kusini yameongezeka na kuchangia "mzozo mkubwa" unaosababisha watu wengi walioondolewa katika makazi yao, wakijaribu kukabiliana na wakati mgumu wakiwa katika mazingira ya vituo vya afya ambavyo havina vifaa vya kutosha.

Kwa muda mrefu Sudan Kusini imekumbwa na ukosefu wa usalama na hali tete ya kisiasa, lakini mvutano kati ya Rais Salva Kiir na makamu wake, Riek Machar, umesababisha mgawanyiko zaidi na mapigano ya makundi yao kote nchini katika miezi ya hivi karibuni.

Jamii ya kimataifa imeangazia zaidi katika mapigano ya jimbo la Upper Nile, lakini MSF inaonya kuwa mapigano yalikuwa yanatokea katika majimbo ya Jonglei, Unity, na jimbo la Magharibi ya Kati la Equatorial.

"Tunazungumzia mzozo mkubwa ambao unatokea katika kila eneo na vijiji," Meneja wa shughuli za MSF Bakri Abubakr amesema.

'Mzozo mkubwa'

Abubakr ameelezea kuhusu watu kuhamishwa kutoka makazi yao kama "mzozo mkubwa" – huku watu karibu 60,000 wakiondolewa katika jimbo la Upper Nile na 50,000 katika jimbo la Jonglei pekee.

Maafisa wa MSF wameshuhudia vijiji vizima ambavyo watu wameondolewa, alisema, akieleza kuwa "hospitali, vituo vya afya na maeneo ya kijamii vimekimbiwa ikiwemo na maafisa wao pia."

"Tunachoshuhudia ni kusambaratika kwa mfumo wa afya nchini humo," alisema, akiongeza kuwa ni nusu tu ya vituo vya afya vya Sudan Kusini ambavyo vilikuwa vinafanya kazi hata kabla ya mapigano ya hivi sasa.

Karibu 80% ya mfumo wa afya wa nchi hiyo unafadhiliwa na mashirika ya kimataifa, MSF imesema, huku Juba ikichangia 1.3% kutoka kwa bajeti yake.

Mashambulizi kwa vituo vya afya

"Tunaona kuwa mashambulizi yameongezeka dhidi ya vituo vya afya, na wahudumu wa afya, raia," amesema Abdalla Hussein wa MSF, ikiwemo mashambulizi dhidi ya maboti katika mto wa White Nile ambayo yalikuwa yanasafirisha dawa na vifaa vingine muhimu.

Umoja wa Mataifa unasema wahudumu wanane wa afya wameuawa mwaka huu, na MSF inaamini idadi huenda ikawa kubwa zaidi.

Mkuu wa ofisi ya MSF Zakariya Mwatia ameeleza kuhusu idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa ambao wanawasili katika mji wa Malakal baada ya wiki kadhaa za kulala katika sehemu mbaya na kusafiri kwa njia ya msituni, hali yao ya afya ikiwa imezorota – na wahudumu wakishindwa kuwaokoa.

"Bado hali ni tete," aliongeza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#