Dollar

40,6712

0.08 %

Euro

46,4201

-0.18 %

Gram Gold

4.308,5800

0.21 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kenya imewasilisha malalamiko rasmi kuhusu masharti mapya ya biashara na leseni yaliyotangazwa na Tanzania wiki hii.

Serikali ya Kenya yalalamika kuhusu masharti mapya ya biashara Tanzania

Kenya inaonya masharti mapya ya kufanya biashara Tanzania na upatikanaji wa leseni kuwa yanaweza kutatiza uhusiano wa kiuchumi katika kanda na kukiuka misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa biashara wa Kenya Lee Kinyanjui ameeleza wasiwasi wake kuhusu sheria ya Fedha 2025 na masharti mapya kuhusu leseni za biashara. Kinyanjui anasema kuongezwa kwa kodi kwa wasiokuwa raia wa Tanzania ni ubaguzi wa kibiashara.

Masharti hayo ya Tanzania yamepiga marufuku kwa wasiokuwa raia kufanya biashara zinazoaminika kuwa ndogo ndogo nchini humo ikiwemo zile za miamala ya pesa, saluni, mikahawa, pamoja na uongozaji wa watalii.

Baadhi ya wafanyabiashara nchini Kenya wamelalamikia hatua hiyo wakiona kama inalenga biashara zao.

Wanaharakati na raia nchini Kenya wametaka serikali yao ilipize kwa kuchukuwa hatua kama hizo dhidi ya raia wa Tanzania.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#