Sport
Dollar
40,7015
0.02 %Euro
47,2204
1.43 %Gram Gold
4.394,9300
2.22 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Maafisa wa usalama wanasema kumekuwa na mashambulizi mapya kutoka kwa wapiganaji katika mkoa wa Cabo Delgado
Wanakijiji wasiopungua watano wameuawa siku ya Alhamisi katika eneo linalokumbwa na mapigano la mkoa wa Cabo Delgado province nchini Msumbiji, kulingana na maafisa wa usalama.
Kamanda wa jeshi katika mkoa huo, Andre Rafael Mahunguane, amewaambia waandishi wa habari kuwa kundi la magaidi liliingia katika kijiji cha Melija wilaya ya Chiure na kuwakusanya wanakijiji kabla ya kuwauwa baadhi yao.
“Lakini baadaye wakakimbia baada ya baadhi ya wanavijiji kuwazidi nguvu. Kwa sasa, watu wameondoka katika kijiji hicho kwa sababu ya hofu kufuatia matukio ya kuwepo kwa mashambulizi mapya ya waasi katika eneo hilo,” amesema Mahunguane.
Makundi mengi yanapigania udhibiti wa eneo hilo lenye utajiri wa madini.
Hivi karibuni wanavijiji pamoja na maafisa wa usalama wameuawa katika eneo hilo. Siku chache zilizopita, maafisa wawili wa polisi waliuawa na wanakijiji katika tukio la kushindwa kuwatambua, amesema Mahunguane.
“Maafisa hao wa polisi walienda katika vijiji wakifanya msako usiku, lakini wanavijiji wakawaua, kwa sababu walidhani ni magaidi. Baadaye waligundua kuwa ni maafisa wa polisi waliokuwa kwenye doria,” alisema.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) linasema watu zaidi ya 25,000 wameondolewa katika makazi yao katika siku za hivi karibuni kwenye eneo hilo. na kufanya idadi kuwa jumla ya watu milioni 1.3 kwa wale wote walioondolewa kwenye vijiji vyao tangu 2017.
Comments
No comments Yet
Comment