Sport
Dollar
40,7015
0.02 %Euro
47,2204
1.43 %Gram Gold
4.394,9300
2.22 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mwaka jana, madai kama hayo yaliyohusishwa na nabii huyo pia yalienea, yakidai kuwa unabii wake ukitabiri Novemba 2, 2024 kuwa siku ya mwisho.
Mhubiri mashuhuri nchini Kenya anayejiita Nabii David Owuor amekanusha madai ya mitandaoni kwamba alitabiri Agosti 2, 2025 kuwa mwisho wa dunia.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na kanisa lake siku ya Ijumaa, kanisa hilo lilipuuza ripoti zinazosambazwa na kusema ni za uongo na zinaenezwa makusudi ili kuharibu sifa ya mhubiri huyo na kudhoofisha ujumbe wa huduma yake.
"Uongozi wa kanisa unashutumu vikali kuenea kwa habari za uwongo na za kupotosha kuhusu Ulimwengu unaoisha Agosti 2, 2025," taarifa hiyo ilisoma.

Nabii huyo alipata umaarufu alipofanya ibada ya umma mwaka 2013 kabla ya uchaguzi mkuu nchini ambapo naibu Waziri Mkuu na mgombea urais wakati huo Uhuru Kenyatta pamoja na Waziri Mkuu wakati huo Raila Odinga walihudhuria.
Kanisa hilo liliwashutumu wale waliohusika na ripoti hizo kwa kupotosha mafundisho ya nabii huyo ili kulidharau kanisa.
"Madai haya yanalenga kudhuru sio tu sifa ya nabii wa bwana, Dkt David Owuor, na kanisa lake, lakini pia umoja na ushuhuda wa kanisa letu," taarifa hiyo iliongeza.
Dkt. David Edward Owuor, anayejiita nabii, ni mmoja wa watu mashuhuri wa kidini nchini Kenya hasa kwa sababu anavutia halaiki ya watu kila mara.
Anajulikana kwa mikutano yake mikuu ya hadhara, suti ya pekee ya rangi nyeupe, na wito mkali wa toba, ambao umevutia maelfu ya watu kwenye huduma yake.
Habari za siku hiyo ya mwisho zilizua hofu kwa baadhi ya waumini.
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa habari kama hizo kuibuka mtandaoni.
Mwaka jana, madai sawa na hayo yaliyohusishwa na nabii huyo pia yalienea, yakidai kuwa unabii wake ulisema kwamba Novemba 2, 2024 itakuwa siku ya mwisho.
Comments
No comments Yet
Comment