Sport
Dollar
40,7015
0.02 %Euro
47,2204
1.43 %Gram Gold
4.394,9300
2.22 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Michuano hiyo, ambayo ni maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani, inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.
Mashindano ya CHAN 2024 yamebisha hodi kwenye ardhi ya Afrika Mashariki na taswira ya timu zinazotoka ukanda huo iko hivi.
Tanzania watakuwa wakifungua dimba la michuano hii, watakapopepetana na Burkina Faso, katika mchezo wa Kundi B, utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Licha ya kuwa nyumbani, ‘Taifa Stars’, inayoongozwa na Hemed Suleiman Ali maarufu kama Morocco, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Wabukinabe, wenye kushika nafasi ya 63 kwa ubora wa soka duniani.

Tanzania, ambayo pia ipo kundi moja na Madagascar, Mauritania na Jamhuri ya Afrika ya Kati, inashika nafasi ya 103 ulimwenguni.
Yote tisa, kumi ni mtiti utakaoibuka kwenye Kundi A, ambako Kenya watajaribu kutumia viwanja vya Moi Kasarani na Nyayo, kurudisha imani ya wapenda soka kwa timu ya Harambee Stars, ambayo kwa kiasi fulani wameikatia tamaa timu yao ya taifa inayoongozwa na nyota wa zamani wa Porto na West Ham United, Benni McCarthy.
Ama kwa hakika, itakuwa ni patashika nguo kuchanika ndani ya kundi hilo, wakati ambapo Harambee Stars, yenye kushika nafasi ya 109 duniani, itakapofungua dimba na DRC, wababe wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Haitokuwa michuano rahisi kwa Kenya, ambayo hivi karibuni ilisusia michuano maalumu ya mataifa manne iliyofanyika nchini Tanzania, kwani bado watakuwa na kibarua kigumu cha kuvuka viunzi vya wababe wa soka Afrika, timu ya Morocco, bila kuwasahau Zambia na Angola.
Kama ulikuwa hujui, Morocco na DRC wameshawahi kutwaa kombe la CHAN mara mbili, hapo awali.
Ikishika nafasi ya 88 duniani, Uganda Cranes watakuwa na mtihani wa kutoboa mbele ya Niger, Guinea Algeria na Afrika Kusini katika kundi C.

Licha ya kutumia uwanja wa nyumbani wa Mandela wa jijini Kampala, vijana wa Paul Put watawakaribisha mashujaa wa jangwa, timu ya taifa ya Algeria siku ya Agosti 4, katika mechi ya ufunguzi wa kundi C.
Hata hivyo, haitokuwa rahisi kwa The Cranes, haswa ukizingatia kuwa wanavaana na mabingwa wa zamani wa AFCON na timu inayoshika nafasi ya 36 duniani, yaani kule anakotokea nyota wa zamani wa Manchester City, Riyad Karim Mahrez.
Siku nne baadaye, Uganda wataikaribisha Guinea, kisha Niger kabla ya kumaliza na Bafana Bafana ya Afrika Kusini.
Hii itakuwa ‘ngodo igwa’ kwa Uganda.
Michuano hiyo, ambayo ni maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani, inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.
Comments
No comments Yet
Comment