Dollar

40,6560

0.04 %

Euro

47,0371

1.13 %

Gram Gold

4.373,2500

1.71 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tamko hilo linakuja siku chache baada ya Tanzania kupiga marufuku raia wa kigeni kumiliki na kuendesha biashara ndogondogo, hatua iliyozua wasiwasi na upinzani kutoka nchi jirani ya Kenya.

Jumuiya ya EAC yazitaka nchi wanachama kuheshimu mpango wa soko la pamoja

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Nduva, amezitaka nchi wanachama za jumuiya kutekeleza mikataba yenye kuheshimu mpango wa soko la pamoja kwa ajili ya kufikia utangamano wa kikanda.

Katibu Mkuu huyo amezitaka nchi hizo kuheshimu mikataba na maazimio hayo ili kulinda soko la kanda ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tamko hilo linakuja siku chache baada ya Tanzania kupiga marufuku raia wa kigeni kumiliki na kuendesha biashara ndogondogo, hatua iliyozua wasiwasi na upinzani kutoka nchi jirani ya Kenya.

“Ni muhimu kuzikumbusha nchi wanachama kuwa si vyema kurudi nyuma kwenye maazimio yaliyo chini ya itifaki ya soko la pamoja,” alisema Nduva katika taarifa hiyo.

Kulingana na Nduva, itifaki hiyo inazitaka nchini wanachama kutozuia sekta na biashara mbalimbali ambazo zimeruhusiwa na kuidhinishwa na jumuiya ya EAC.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa sekretariati ya EAC, kwa sasa inafanya tathmini ya utekelezwaji wa itifaki hizo na ikibidi, itatoa ripoti kuhusu namna baadhi ya nchi wanachama zinavyokiuka mikataba hiyo.

Kauli hiyo ya EAC inakuja siku chache baada ya Tanzania kutoa agizo la kukataza wageni kushiriki katika sekta 15 zikiwemo uhamishaji wa pesa kwa njia ya simu, uongozi wa watalii, uchimbaji mdogo wa madini, ununuzi wa mazao shambani, saluni za urembo, maduka ya bidhaa za kiutamaduni, pamoja na kuanzisha redio na televisheni.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa nchi hiyo, Dkt. Selemani Jafo, alisema kuwa wageni wamekuwa wakijihusisha kwa kasi na sekta isiyo rasmi na maeneo ambayo yanafaa zaidi kuachiwa Watanzania.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#