Dollar

40,6558

0.04 %

Euro

46,9071

0.86 %

Gram Gold

4.375,4100

1.76 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Hii ni baada ya mwindaji mmoja nchini humo kumuua Simba anayedaiwa kutumika kwa utafiti wa wanyamapori.

Mauaji ya Simba wa utafiti yazua utata nchini Zimbabwe

Wadau wa uhifadhi nchini Zimbabwe wameoneshwa kukerwa na mauaji ya simba mmoja aliyekuwa amevalishwa cola, kwa sababu za kiutafiti.

Tukio hilo, ambalo lilimhusisha mwindaji wa wanyamapori huko Zimbabwe, limeibua kumbukumbu za simba aliyefahamika kama Cecil, ambaye aliuwawa na watalii kutoka Marekani, miaka 10 iliyopita.

Blondie, simba aliyekuwa amefungwa cola shingoni, alikuwa ni sehemu ya utafiti wa Chuo Kikuu cha Oxford, zoezi lililokuwa limesimamiwa na kampuni ya utalii ya Africa Geographic.

Inadaiwa kuwa, Blondie aliuwawa mwezi Juni, karibu na Hifadhi ya Taifa ya Hwange, baada ya kuhadaiwa kutoka eneo la hifadhi hadi kwenye eneo la kuwindia wanyama.

Kufuatia malalamiko kutoka kada ya uhifadhi, msemaji wa Hifadhi za Taifa Zimbwabwe, aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa zoezi hilo ‘lilifanyika kihalali’, akiongeza kuwa mwindaji alikuwa na kibali halali cha kumuwinda mnyama huyo.

Kila mwaka, Zimbabwe hutoa kibali cha kuvuna simba 100, huku wawindaji wabobezi wakilipa fedha nyingi kwa ajili kuwinda simba na kuondoka na kichwa au ngozi zao kama kumbukumbu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#