Sport
Dollar
38,7514
-0.1 %Euro
43,4837
0.04 %Gram Gold
3.963,3900
-2.23 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Ufafanuzi huo umekuja huku kukiwa na ongezeko wa malalamiko kutoka kwa wananchi, viongozi wa kisiasa kuhusu ukodishaji wa viwanda vya sukari vinavyomilikiwa na Serikali, baadhi ya viongozi wakiibua wasiwasi juu ya uwazi na ushirikishwaji wa wananchi.
Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa hakuna kiwanda cha sukari nchini Kenya ambacho kimeuzwa, na kufafanua kuwa serikali imevikodisha tu kupitia mchakato wa uwazi, ulioidhinishwa na Bunge.
"Ukodishaji uliidhinishwa na Bunge, na hakuna kiwanda kilichouzwa. Tumejitolea kwa uwazi kamili," alisema Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe.
Ufafanuzi huo umekuja huku kukiwa na ongezeko la malalamiko kwa wananchi, viongozi wa kisiasa kuhusu ukodishaji wa viwanda vya sukari vinavyomilikiwa na Serikali, huku baadhi ya viongozi wakiibua wasiwasi juu ya uwazi na ushirikishwaji wa wananchi.
Akifika mbele ya Kamati ya Idara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Waziri Kagwe alisisitiza kuwa wadau wote walihusishwa na kwamba serikali iko tayari kuwasilisha nyaraka zozote kwa ajili ya uchunguzi.

"Marekebisho ya sekta ya sukari ni mambo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa muda mrefu ndani ya Bunge hili, Bunge lenyewe lilikuwa limeunda kikao cha sukari na ndilo lililojadili suala la kuuza au kukodisha viwanda hivyo na hatimaye kuamua kuvikodisha," alisema.
Kulingana na Waziri huyo mchakato wa ukodishaji ndio uamuzi bora zaidi wa kuokoa kampuni zilizo katika hali mbaya kwani wazalishaji binafsi watarekebisha viwanda na kulinda ustawi wa wakulima na wafanyakazi.
Makampuni yaliyokodeshwa
Katika ukodishaji wa hivi majuzi, Kampuni ya Sukari ya West Kenya ilichukua Kampuni ya Sukari ya Nzoia, huku Kibos Sugar na Allied Industries Ltd zikikabidhiwa kwa Kampuni ya Chemelil Sugar, zote kwa kandarasi ya miaka 30.
Kampuni ya Sukari ya Sony, kwa upande mwingine, ilikodishwa kwa Viwanda vya Sukari vya Busia, na West Valley Sugar Company Ltd itashughulikia Kampuni ya Sukari ya Muhoroni.
"Wakulima wa miwa nchini wanadai malipo ya zaidi ya dola milioni 43 ambayo ni takriban shilingi bilioni 5.6, na jambo la kushangaza ni kwamba tuna kiwanda kimoja ambacho kinaendeshwa na sekta kibinafsi ambacho hulipa wakulima kila wiki, hulipa kodi ... si kamili, lakini angalau huwalipa wafanyakazi wao kila wiki," Waziri Mutahi alisema.
"Madeni yote ya wakulima yalichukuliwa na serikali; hakuna mkulima atakayeteseka. Isipokuwa ni kama umekodisha madeni hayo, madeni hayo yanayodaiwa na wakulima yanaweza kugeuka kuwa madeni mabaya. Tulichofanya kwa kuchagua chaguo la kukodisha ni kubadili madeni mabaya ya wafanyakazi kuwa akaunti zinazopokelewa."
Waziri huyo pia alihakikisha kuwa maslahi ya wakulima yanasalia kuwa kipaumbele, huku serikali ikishughulikia madeni ambayo bado yanadaiwa kwao na wafanyakazi.
Kikao hicho kilimalizika kwa wabunge kuonyesha imani na mchakato wa mageuzi yanayolenga kufufua sekta ya sukari.
Comments
No comments Yet
Comment