Sport
Dollar
38,8220
-0.01 %Euro
43,6190
0.33 %Gram Gold
3.964,9500
-2.19 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Waafrikaner waliondoka kwa sababu wanapinga sera zinazolenga kushughulikia tatizo la ubaguzi wa rangi.
Kanisa moja nchini Marekani limekataa kuwapa hifadhi raia wa Afrika Kusini wazungu wanaojulikana kama Afrikaner, ambao wamepelekwa nchini humo na serikali ya Rais Donald Trump kwa madai kwamba wananyanyaswa nchini mwao. Afrika Kusini ina sheria mpya inayoipa serikali uwezo wa kuchukua ardhi kwa ajili ya manufaa ya umma.
Mpango huo, una nia ya kupunguza hali ya kundi moja kuhodhi ardhi kubwa zaidi huku wengine wakiwa hawana kabisa.
Sheria hii mpya inafuta ile ya awali ya wakati wa ukoloni wa nchi hiyo na awamu ya ubaguzi wa rangi ambapo ardhi ilipewa watu kulingana na rangi zao.

Hivyo, Wazungu wa Afrika Kusini wakapata zaidi. Mwezi Februari, 2025 Rais Trump alitangaza atawapa makazi raia hao wa Afrika Kusini kwa madai kuwa, sheria hiyo ya ardhi inalenga kusaidia serikali kunyakua ardhi yao.
Hivyo, kukata misaada yote ya kifedha kwa Afrika Kusini, huku akitaka kutoidhinishwa kwa sera yake ya ardhi na wakati huo huo, akipinga kesi ya mauaji ya halaiki iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Mpaka sasa, WaAfrikaner 59 tayari wamewasili nchini Marekani mwanzoni mwa wiki.
Changamoto ya makazi
Lakini Kanisa la Episcopal nchini Marekani limesema zaidi ya wiki mbili zilizopita, kuwa serikali ya Marekani ililifahamisha kwamba chini ya masharti ya ruzuku ambayo Marekani inawapa wanatarajiwa kuwapa makazi wakimbizi hao kutoka Afrika Kusini.
Hata hivyo, askofu wa kanisa hilo katika taarifa yake amesema kuwa inasikitisha kuona kundi moja la wakimbizi, waliochaguliwa kwa namna isiyo ya kawaida, wakipendelewa kuliko wengine ambao wamekuwa wakisubiri kwa miaka katika kambi za wakimbizi au mazingira hatarishi.
Kwa upande wake, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Waafrikaner waliondoka kwa sababu wanapinga sera zinazolenga kushughulikia ubaguzi wa rangi.
Tumeibua wasiwasi wetu wenyewe kwa sababu wale watu ambao wameshawishiwa kwenda Marekani hawalingani na ufafanuzi wa mkimbizi,” Rais Ramaphosa alisema akiwa katika Mkutano wa kongamanao wa kiuchumi Afrika uliofanyika Côte d'Ivoire tarehe 12 na 13 Mei.
Inaripotiwa kuwa, Waafrikaner bado wanamiliki robo tatu ya ardhi binafsi na wana utajiri takriban mara 20 ya waafrika weusi wa nchi hiyo.
Wazungu wengine wa Afrika Kusini wameendelea kujisajili kwa lengo la kutaka kupelekwa nchini Marekani kama wakimbizi, huku wengine wakikataa.
Mpango huu wa Tump, unaonekana kukinzana na sera zake za awali za kutaka kuwaondoa mamilioni ya wahamiaji ambao tayari wapo nchini mwake kwa miaka kadhaa.
Comments
No comments Yet
Comment