Dollar

38,8164

0.02 %

Euro

43,5375

0.09 %

Gram Gold

4.049,2200

-0.11 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Upigaji kura unatarajiwa kufanyika tarehe tano mwezi Juni, 2025

Kampeni za uchaguzi zaanza rasmi nchini Burundi kwa wabunge, serikali za mitaa

Kampeni za uchaguzi kwa wabunge na serikali za mitaa nchini Burundi zimeanza rasmi siku ya Jumanne.

Kampeni hizo zitaendelea hadi tarehe 2 Juni, siku tatu kabla ya upigaji kura, ambao utakuwa tarehe 5, Juni.

Ishara ya hafla ya kuzindua kampeni hizo ilifanyika eneo la Gitega siku ya Ijumaa, mji mkuu wa kisiasa wa taifa hilo, na Rais Evariste Ndayishimiye pia alihudhuria.

Bunge la Burundi lina jumla ya viti 123, wabunge 100 wanachaguliwa na wananchi moja kwa moja na wale wa kujaza nafasi hizo wakiwakilisha mashirika na makundi mbalimbali.

Chama cha Ndayishimiye cha National Council for the Defense of Democracy–Forces for the Defense of Democracy (CNDD–FDD) kilipata wingi wa wawakilishi katika uchaguzi uliopita wa 2020.

Chama hicho, kiloanzishwa 1998 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi, kimekuwa madarakani tangu 2005.

Tarehe 23 Julai kutafanyika uchaguzi wa bunge la Seneti katika nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni 13.5.

Ni mwaka wenye shughuli nyingi barani Afrika huku nchi tisa zikitarajiwa kufanya uchaguzi wa urais na uchaguzi wa wabunge ukifanyika katika mataifa saba.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#