Sport
Dollar
38,8091
0.04 %Euro
43,4915
0.98 %Gram Gold
4.057,5900
0.55 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Watu zaidi 84,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Somalia tangu katikati mwa mwezi Aprili, Umoja wa Mataifa umesema, huku idadi ya waliofariki ikifikia 17.
Watu zaidi ya 84,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Somalia tangu katikati mwa mwezi Aprili, Umoja wa Mataifa umesema siku ya Jumanne, na kusababisha vifo vya karibu watu 17.
Eneo hilo ni moja ya maeneo ambayo yameharibiwa na mabadiliko ya tabianchi, na matukio ya hali mbaya ya hewa.
"Tangu katikati mwa mwezi Aprili, mafuriko yamesababisha watu 17 kufariki na kutatiza maisha ya watu zaidi 84,000 katika maeneo mbalimbali," Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na misaada kwa watu OCHA limesema.
Idadi hiyo inajumuisha watu ambao wameondolewa kwenye makazi yao, wamepoteza maeneo ya kuishi, na sasa hawana sehemu ya kupata msaada, au wanakabiliwa na uhaba wa maji.
Miundombinu imeharibiwa
Majimbo ya Jubaland, Hirshabelle,Kusini Magahribi, Galmudug, Puntland na eneo la Banadir – ambayo yanajumuisha mji mkuu Mogadishu – yaliathirika zaidi, OCHA imesema, na kuacha watu zaidi ya 8,100 bila makazi.
"Miundombinu muhimu imeharibiwa," imeongeza, ikieleza kuwa maeneo ya maji pia yamefunikwa na mafuriko na mashimo ya vyoo karibu 200 pia yameharibiwa.
Haya yanatokea siku kadhaa baada ya mvua kubwa kusini mashariki kwa Banadir kusababisha vifo vya watu wasiopungua tisa na kutatiza maisha ya wengine karibu 24,600.
"Mvua zimeathiri sana watu ambao walipoteza makazi yao," OCHA ilisema, ikiwanukuu mamlaka za serikali za mitaa.
Mvua zaidi zinatarajiwa
Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, wataalamu wa hali ya hewa wanaonya kuwa kutakuwa na mvua zaidi katika siku zijazo kote kusini na katikati mwa Somalia.
Somalia ilikumbwa na mafuriko mwaka 2023. Watu zaidi ya 100 walifariki na wengine zaidi ya milioni moja kuachwa bila makazi yao kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Nino.
Comments
No comments Yet
Comment