Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Kundi la Madaktari nchini Sudan limesema kwamba wapiganaji wa RSF wameigeuza Hospitali ya Al-Nuhud kuwa kituo cha kijeshi, hatua iliyowalazimu wahudumu wa afya kukimbia na kuwaacha raia bila huduma muhimu.

RSF nchini Sudan watuhumiwa kuigeuza hospitali ya Kordofan Magharibi kuwa kambi ya kijeshi

Kulingana na kundi hilo, RSF iligeuza sehemu kubwa ya hospitali hiyo kuwa kituo cha maelekezo ya kijeshi na sehemu na makazi wanajeshi baada ya kuuteka mji huo zaidi ya miezi mitano iliyopita. Hii imesababisha hospitali kushindwa kutoa huduma za msingi kwa wakazi.

Kundi hilo limeonya kuwa kutumia kituo cha afya kwa madhumuni ya kijeshi ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na kunatishia haki ya raia kupata huduma za afya.

Limesema pia kuwa wahudumu kadhaa wa afya katika hospitali ya Al-Nuhud walikabiliwa na unyanyasaji na kutuhumiwa kuiunga mkono jeshi la Sudan, hali iliyowafanya wengi wao kukimbia. Kwa sasa hospitali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi.

Kwa mujibu wa kundi hilo, huduma zilizobaki ni chache sana, na kuwekewa kipaumbele kwa wanachama wa RSF katika idara nzima ya dharura kumeifanya hospitali hiyo kufanana kikamilifu na kambi ya kijeshi, na kuwaacha raia bila huduma muhimu.

Kundi hilo la madaktari limesema lina wasiwasi kuhusu maelfu ya wakazi waliobaki mjini humo na ambao sasa wanapata ugumu mkubwa kupata huduma za afya.

Limetaka RSF kuondoka mara moja katika Hospitali ya Al-Nuhud, kuirejesha kwa matumizi ya raia, kuwalinda wahudumu wa afya na kurejesha huduma za msingi bila ubaguzi.

RSF haijatoa maoni yoyote kuhusu tuhuma hizi.

RSF iliteka mji wa Al-Nuhud mwezi Mei baada ya mapigano makubwa na jeshi la Sudan. Mapigano kati ya pande hizo mbili yameongezeka katika majimbo yote matatu ya Kordofan wiki za karibuni, na kusababisha makumi ya maelfu ya raia kukimbia makazi yao.

Kwa sasa RSF inadhibiti majimbo yote matano ya Darfur, huku jeshi likishikilia majimbo mengi yaliyobaki 13, ikiwemo Khartoum.

Darfur inachukua takriban sehemu moja ya tano ya ardhi ya Sudan, lakini idadi kubwa ya wakazi milioni 50 wa nchi hiyo wanaishi katika maeneo yanayodhibitiwa na jeshi.

Mgogoro kati ya jeshi la Sudan na RSF ulioanza Aprili 2023 tayari umesababisha vifo vya angalau watu 40,000 na kuwahamisha watu milioni 12, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#