Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Senegal imethibitisha kuwa Embalo aliwasili mjini Dakar "akiwa salama" baada ya mapinduzi kuzuia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi nchini Guinea-Bissau.

Rais wa Guinea-Bissau awasili Senegal baada ya jeshi kufanya mapinduzi

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo amewasili nchini Senegal baada ya kuzuiwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi nchini kwake, serikali ya Senegal imesema siku ya Alhamisi.

“Ndege ilikodishwa na serikali ili kusafiri hadi Bissau kwa lengo la kusaidia katika operesheni hii. Hii imesaidia kufika kwa Rasis Umaro Sissoco Embalo akiwa salama nchini Senegal,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Senegal ilisema katika taarifa.

Mapema siku ya Alhamisi jeshi la Guinea-Bissau lilimteua Jenerali kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo, siku moja baada ya mapinduzi na kusitisha kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Mgombea wa upinzani Fernando Dias da Costa ameiambi AFP kuwa anaamini kuwa alishinda uchaguzi wa Jumapili na kudai Embalo — ambaye anadai ameshinda — "alipanga" mapinduzi kumzuia yeye asiingie madarakani.

Mapinduzi yamekuja siku moja kabla ya matokeo ya muda ya uchaguzi wa urais na ubunge kutangazwa.

Jenerali Horta N’Tam, mkuu wa majeshi, alitangazwa kuwa kiongozi wa nchi kwa mwaka mmoja.

Alikula kiapo katika makao makuu ya jeshi, akitangaza: "Nimeapishwa kuongoza Baraza Kuu."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#