Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi.

Wabunge wa Afrika Mashariki wapongeza ushindi wa Rais Samia

Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Wakizungumza wakati wa kikao cha bunge hilo, kinachofanyika jijini Kampala Uganda, wajumbe hao walisema kuwa ushindi wa Samia ni dhihirisho la kielelezo cha mwanasiasa huyo, kuwa mfano kwa wanawake wengine barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

“Amekuwa ni kielelezo na mfano  kwa wanawake wengi duniani kwa kuwa kati ya wanawake wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya urais,” alisema Jacqueline Amongin mbunge wa EALA kutoka Uganda.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Makame Hasnuu.

“Hususani wanawake wanapozidi kung’aa katika nafasi za uongozi, hii inakuwa fahari na furaha kwa wanawake wote ambao ambao hawakuwahi kufikiria kushika nyadhifa ya juu kama ya urais,” alisema mbunge.

Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#