Dollar

38,8546

0.35 %

Euro

43,3112

-0.43 %

Gram Gold

3.983,4900

-1.24 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo, aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi mwaka 2023, amesafiri kwa ndege hadi Angola pamoja na mkewe na mwanae, ambao walihamishwa kutoka jela hadi kifungo cha nyumbani wiki iliyopita.

Rais wa zamani wa Gabon aelekea Angola na familia yake

Ofisi ya Rais wa Angola imesema katika taarifa yake iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kwamba Rais wa zamani wa Gabon, Ali Bongo amesafirishwa na familia yake kuelekea Angola.

Maafisa wa Umoja wa Afrika walitoa wito mwezi uliopita kuachiliwa kwa mke wa Bongo, Sylvia Bongo, 62, na mwanae Noureddin, 33, ambao waliwekwa chini ya ulinzi muda mfupi baada ya mapinduzi ya Agosti 2023 na kutuhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na ubadhirifu na utakatishaji fedha.

Ali Bongo mwenyewe, ambaye ana umri wa miaka 66, awali aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya mapinduzi hayo ingawa maafisa baadaye walisema aliruhusiwa kuhama nchi na kwenda anapotaka. Hata hivyo, wafuasi wake walisema hili si kweli na hajulikani kama aliondoka ikulu ya rais ya Libreville tangu wakati huo.

Vyanzo viwili vinavyofahamu kisa hicho vililiambia Shirika la Habari la Reuters kwamba familia hiyo iliondoka Gabon kabla ya saa sita usiku Alhamisi.

Sylvia na Noureddin Bongo walihamishiwa katika kifungo cha nyumbani Mei 9. Hivi majuzi walikuwa wamezuiliwa katika vyumba vya chini ya ardhi katika ikulu ya Rais huko Libreville, mmoja wa vyanzo vinavyofahamu kesi hiyo alisema.

Wafuasi wao wamesema waliteswa wakiwa kizuizini, ingawa kiongozi wa mapinduzi Brice Oligui Nguema, ambaye sasa anahudumu kama rais, amekanusha hilo.

Waziri wa mawasiliano wa Gabon, Paul-Marie Gondjout, hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni yake. Nguema aliapishwa kwa muhula wa miaka saba kama rais mwezi huu baada ya kushinda uchaguzi kwa karibu 95% ya kura.

Katika mkutano wa Aprili 30, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika liliirejesha Gabon AU, ambayo uanachama wake ulikuwa umesitishwa baada ya mapinduzi.

Katika taarifa yake, baraza hilo limetaka kuachiliwa mara moja kwa familia ya Ali Bongo na kuhakikishiwa kuwa haki na afya zao zitalindwa.

Bongo alikuwa ametawala Gabon tangu 2009, akichukua nafasi ya babake, ambaye alifariki baada ya zaidi ya miongo minne madarakani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#