Dollar

38,8562

0.35 %

Euro

43,2635

-0.52 %

Gram Gold

3.976,5600

-1.41 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia imedai kuwa TPLF imeshindwa kutekeleza "hatua za marekebisho" zinazotakiwa.

Chama cha TPLF Ethiopia chailalamikia AU baada ya kufutiwa usajili na Tume ya Uchaguzi

Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) nchini Ethiopia kimetoa ombi la dharura kwa Umoja wa Afrika (AU) kufuatia uamuzi wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Ethiopia (NEBE) kukifutia hadhi yake ya kisheria.

Chama hicho cha kaskazini mwa nchi ndicho kilichopigana na jeshi la Ethiopia kati ya 2022 na 2022 kaskazini mwa nchi hiyo.

Vita hivyo, vilichukua maisha ya watu 600,000 na kusababisha zaidi ya watu milioni 3 kuyahama makazi yao kulingana na takwimu.

Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia imedai kuwa TPLF imeshindwa kutekeleza "hatua za marekebisho" zilizoagizwa.

Imedai kuwa TPLF haikutimiza masharti ya usajili wake maalum, ambayo yalitaka chama kufanya mkutano mkuu ndani ya miezi sita ya usajili wake wa Agosti 2024 chini ya hadhi maalum, na kuiarifu Bodi siku 21 kabla.

Hii ni licha ya tahadhari iliyotolewa mwezi Februari.

TPLF imeambia AU katika barua yake kwamba uamuzi huo wa Tume ya Uchaguzi ni ukiukaji wa moja kwa moja wa Makubaliano ya Pretoria ya 2022. Haya ni makubaliano ya amani yaliyofanywa na serikali ya Ethiopai na chama hicho kumaliza vita vya miaka miwili kaskazini mwa nchi.

Barua imetiwa saini na Mwenyekiti wa TPLF Dkt. Debretsion Gebremichael.

Katika barua rasmi iliyotumwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya AU Mahmoud Ali Youssouf, TPLF ilielezea hatua ya tume ya uchaguzi kama "uvunjaji wa kimsingi" wa makubaliano ya amani ambayo yalimaliza vita vya miaka miwili huko Tigray.

TPLF ilionya kwamba kukiita kikundi hicho "chama haramu cha kisiasa" kunatishia mchakato mzima wa amani na kunadhoofisha vifungu vya utambuzi wa pande zote muhimu katika makubaliano.

"Uamuzi wa upande mmoja unainyima TPLF haki iliyokuwa imejipatia kupitia Mkataba wa Pretoria na unaleta tishio kubwa kwa msingi wa mchakato wa amani," barua hiyo ilisema.

TPLF iliitaka AU kuitisha kikao cha dharura ili kupatanisha mzozo kuhusu huo.

Pia imeitaka AU iishinikize serikali ya Ethiopia kusimamisha uamuzi wa Tume ya Uchaguzi hadi mashirika ya AU yatakapotoa muongozo unaolingana na Mkataba wa Kukomesha Uhasama.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#