Dollar

38,8545

0.34 %

Euro

43,3392

-0.36 %

Gram Gold

3.983,7500

-1.24 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Uganda Yoweri Museveni bado hajatamka lolote baada ya ujumbe wa mitandaoni ya mtoto wake ambaye anajulikana kwa kutoa matamko mara kwa mara yenye utata mtandaoni.

Mkuu wa Jeshi Uganda awatisha mabalozi wasiomuunga mkono baba yake

Mkuu wa Jeshi la Taifa la Uganda, UPDF, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametishia kuwafukuza mabalozi walio nchini Uganda ambao hawatamuunga mkono katika Uchaguzi Mkuu Rais Yoweri Museveni.

“Mimi Muhoozi Kainerugaba, mwine Museveni, nina uwezo katika nchi hii KUFUKUZA Balozi yeyote nisiyempenda!” aliandika katika akaunti yake ya X.

Kainerugaba ni mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na aliteuliwa na baba yake kuongoza Jeshi la nchi hiyo mwezi Machi 2024.

Kainerugaba pia alionesha kutoridhishwa na picha iliyomuonyesha balozi wa Umoja wa Ulaya alipokutana na kiongozi wa chama cha Upinzani nchini humo Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine.

“Katika uchaguzi huu unaokuja, wazungu katika nchi yetu wasiomuunga mkono Mzee kwa moyo wote bora wawe makini sana! Tutawafukuza wasaliti wote hadharani!! aliongezea.

Akisema kuwa atamchukulia hatua balozi wa muungano huo.

“Nimeongea na Mzee (akiashiria Rais Museveni) atatangaza vikwazo dhidi ya Umoja wa Ulaya nchini Uganda, watalipia mtazamo wao kwa nchi yetu,” Jenerali huyo alisema kupitia mtandao wa X.

Uganda inapanga kufanya Uchaguzi Mkuu Januari 2026 na Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa Rais tangu 1986 anatarajiwa kugombea tena. Tayari kiongozi wa chama cha NUP, Bobi wine ametangaza kugombea kiti hicho.

Kwa Bobi Wine, iwapo atashiriki, hii itakuwa ni mara yake ya pili kuwania nafasi hiyo. Ingawa katika uchaguzi wa 2021, alishindwa na mpinzani wake Rais Museveni.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda bado hawajatoa tamka lolote kuhusiana na vitisho hivyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#