Dollar

38,8618

0.34 %

Euro

43,3213

-0.4 %

Gram Gold

3.989,7700

-1.09 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kuna madini mengi ya bauxite nchini Guinea-Conakry yanayotumika kuzalisha alumini.

Serikali ya kijeshi ya Guinea yachukua migodi 51 baada ya kufuta leseni zao

Serikali ya kijeshi ya Guinea-Conakry imechukua umiliki wa leseni 51 za uchimbaji madini wakati ikijaribu kusimamia migodi ambayo shughuli zake hazijaanza au sehemu ambazo leseni hazitumiki vizuri, waziri wake wa habari amesema.

Fana Soumah ametangaza katika hotuba yake kupitia televisheni Alhamisi jioni kuwa kiongozi wa kijeshi wa Guinea Mamady Doumbouya ametia saini agizo la kuchukua migodi ,ikiwemo bauxite, dhahabu, na almasi.

Migodi hiyo imerejeshwa kwa serikali "bila malipo yoyote," Soumah amesema, akieleza sababu kuwa ni sheria za uchimbaji madini za Guinea kwa kufuta leseni hizo.

Raslimali nyingi

Guinea ina madini mengi ya bauxite duniani, yanayotumika kutengeneza alumini, na kuuzwa kwake nje ya nchi ni muhimu katika sekta ya uzalishaji chuma, hasa nchini China na Urusi.

Awali serikali ilifuta leseni za madini ya bauxite za kampuni ya Kebo Energy SA na Emirates Global Aluminium.

"Shinikizo la serikali ya Guinea kwa sekta ya bauxite linaongezeka," alisema Tom Price, wa kampuni ya Panmure Liberum.

"Tunahisi kuwa serikali ya Guinea inajaribu kukusanya idadi ya makampuni ya nje yanayochimba madini ya bauxite, na kulazimisha sekta hiyo iliyofanyiwa mabadiliko kuwekeza katika mchakato mwingine," aliongeza.

Wawekezaji wasiyo muhimu

Hata hivyo, mdau mwingine anayefahamu shughuli za sekta ya madini za Guinea, ambaye hakutaka kutajwa, alisema kampuni hizo ambazo zimeathiriwa na agizo hilo siyo wawekezaji wakubwa sana.

Mamlaka za Guinea hazikujibu kuhusu maombi yetu ya kutaka wazungumzie hatua wanazochukua.

Agizo linaathiri shughuli za uchimbaji na wale waliopewa leseni kati ya 2005 na 2023. Baadhi ya leseni zilikuwa tayari muda wake umemalizika, huku zingine zikitarajiwa kuendelea kutumika kwa miongo kadhaa.

Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa Afrika Magharibi, ambapo kuna serikali za kijeshi nchini Niger, Mali na Burkina Faso zimeweka udhibiti mkali wa madini tangu 2020 kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa kodi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#