Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, Rais Donald Trump yupo tayari kukutana na Ayatollah Ali Khamenei wa Iran, kama itahitajika.

Rais Donald Trump ‘yuko tayari’ kukutana na Ayatollah Ali Khamenei wa Iran kama itahijatika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema kuwa rais wa nchi hiyo, Donald Trump angependelea kusuluhisha mgogoro kati ya Marekani na Iran.

“Rais amesema kuwa kipaumbele chake ni kufikia makubaliano na Iran. Ni jambo gumu lakini atajaribu. Na ndicho tunachojaribu kufanya kwa sasa,” alisema Rubio katika mahojiano yake na Bloomberg.

Rubio alisisitiza kuwa anafanya kazi “chini ya kiongozi aliye tayari kuonana na mtu yoyote yule”.

“Nina imani kuwa, hata kama Ayatollah (Ali Khamenei) akisema anataka kuonana na Rais Trump, itawezekana tu, si kwa sababu yeye ni Ayatollah, lakini kwa sababu anaona hiyo ndiyo njia sahihi ya kutatua migogoro duniani,” aliongeza.

Alipoulizwa kuhusu madai ya kutumwa kwa manowari ya pili ya kivita katika eneo la Mashariki ya Kati, Rubio alisema kuwa Iran “haitoruhusiwa kujipatia silaha za kinyuklia”, akisema kuwa itakuwa ni tishio kwa Marekani, Ulaya na usalama mpana wa ulimwengu.

“Tunaona ni sahihi kabisa kupeleka vikosi katika eneo hilo kwa kuwa Iran imeonesha nia yake ya kushambulia uwepo wa Marekani katika kanda hiyo,” alisema Rubio.

 

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#