Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine.

Droni za Ukraine zateketeza ghala la mafuta la Urusi

Mashambulizi ya droni za Ukraine yametekeza ghala la mafuta la Urusi katika eneo la kusini la Krasnodar, kulingana na taarifa iliyotolewa na maofisa wa Urusi siku ya Jumapili.

Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine.

Gavana na wa eneo la Krasnodar Veniamin Kondratyev, alisema kuwa shambulizi hilo lilitokea katika hifadhi iliyopo katika kijiji cha Volna.

Eneo hilo, ndimo iliko hifadhi ya mafuta, mkaa na ngano ya Urusi.

"Hali ni mbaya zaidi katika eneo la Volna ambapo tenki la mafuta na hifadhi zingine zimeharibiwa vibaya," alisema Kondratyev.

Kulingana na Kondratyev, watu wawili walijeruhiwa wakati zaidi ya zimamoto 100 wakipambana kuuzima moto huo.

Kwa upande wake, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa, imefanikiwa kutungua droni 88 za Ukraine katika mipaka iliyo kusini mwa nchi hiyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#