Kwa muda mrefu, China imekuwa ikidai umiliki wa eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha.

China yaionya Marekani kuhusu Taiwan

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ameionya Marekani kuhusu kupanga njama dhidi ya Taiwan.

Kulingana Wang Yi, njama hizo za Marekani, zitasababisha ugomvi mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza mjini Munich, Ujerumani wakati wa mkutano wa mambo ya usalama, Wang amesema kuwa kitendo hicho, ni sawa na Marekani ‘kuvuka mstari mwekundu’ wa China.

"Kwa vyovoyote vile, suala hili litaleta ugomvi mkubwa kati ya Marekani na China,” alisema.

Kwa muda mrefu, China inadai kuwa na umiliki na eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#