Sport
Wizara ya mambo ya nje inasema baadahi ya raia wa Nigeria walipelekwa katika uwanja wa vita baada ya kulaghaiwa kutia saini mikataba ya kijeshi.
Nigeria imeonya raia wake dhidi ya kujisajili kwenda kupigana nje ya nchi baada ya taarifa kuibuka kuwa wengine walilaghaiwa kupigana kwa niaba ya Urusi nchini Ukraine, kama ilivyokuwa kwa raia wengine kutoka nchi za bara la Afrika.
Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria imesema katika taarifa siku ya Jumapili kuwa "inaeleza wasiwasi wake mkuwa kuhusu viwango vya matukio ya raia wa Nigeria kusajiliwa kinyume cha sheria kwenda kupigana katika vita nchi za kigeni", bila kutaja Urusi.
"Raia kadhaa wa Nigeria ambao wamejikuta kwenye mtego huo walipelekwa ktika maene ya vita baada ya kurubuniwa kutia saini mikataba ya kijeshi," wizara ilisema katika taarifa.
Katika wiki za hivi karibuni, taarifa zimeonesha kuwa raia wa nchi za Afrika ambao walirubuniwa kwa ahadi za malipo mazuri Urusi walikuwa wanauawa katika mstari wa mbele vitani Ukraine.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi wiki iliopita alitangaza kuwa atasafiri kuelekea Moscow kwa ajaili ya mazungumzo "ya kumaliza kabisa suala hilo na kulitafutia suluhu".
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema wiki iliopita kuwa alijadiliana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuwarudisha raia wa Afrika Kusini waliorubuniwa kupigania vikosi vya Urusi nchini Ukraine.
Ushahidi pia umeibuka nchini Uganda. Ukraine ilisema mwezi Novemba kuwa imetambua watu wasiopungua 1,436 ambao wanapigana kwa niaba ya Urusi na ambao ni raia wa mataifa 36 ya Afrika.
Comments
No comments Yet
Comment