Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre asema mradi huo ni hatua ya kihistoria kuelekea mageuzi ya uchumi wa Somalia.

Somalia yaanza uchimbaji mafuta baharini kwa ushirikiano na Uturuki

Waziri Mkuu wa Somalia, Hamza Abdi Barre, amepongeza kuanza kwa uchimbaji mafuta baharini kwa ushirikiano na Uturuki, akieleza hatua hiyo kuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa taifa hilo. Kauli yake imekuja wakati meli ya uchimbaji ya Uturuki, Cagri Bey, ikielekea Somalia kwa kazi zake za kwanza nje ya nchi.

Barre amesema hatua hiyo ni ishara kwamba rasilimali za asili za Somalia sasa zinaanza kunufaisha taifa baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu. Ameeleza pia kuwa ushirikiano kati ya Somalia na Uturuki chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdogan unaimarika na kuleta matumaini mapya kwa wananchi.

Meli ya Cagri Bey inatarajiwa kuwasili Mogadishu ndani ya siku 45 na kuanza uchimbaji mwezi Aprili katika kisima cha Curad-1. Makubaliano ya mwaka 2024 kati ya nchi hizo yanahusu uchimbaji wa mafuta na gesi baharini na nchi kavu, huku meli ya Oruc Reis tayari ikiwa imekamilisha uchunguzi wa maeneo matatu yenye uwezekano wa mafuta.

Chanzo: TRT Afrika

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#