Dollar

40,5860

-0.48 %

Euro

47,7946

-0.42 %

Gram Gold

4.353,4200

-1.37 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kikosi cha kijeshi cha RSF na washirika wake wameapa kujenga "Sudan Mpya".

Muungano unaoongozwa na RSF watangaza serikali sambamba nchini Sudan

Muungano wa Kisudani unaoongozwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) ulitangaza serikali sambamba siku ya Jumamosi — hatua ambayo inapingwa vikali na jeshi, na inaweza kusababisha mgawanyiko zaidi nchini wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili vikiendelea.

Serikali hiyo, inayoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo wa RSF, ilitangazwa magharibi mwa nchi.

Msemaji wa muungano unaojulikana kama Sudanese Founding Alliance, Alaa El Din Nugud, alisema katika taarifa ya video iliyorekodiwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa muungano huo siku ya Jumamosi kwamba chombo cha uongozi kiliamua kuanzisha "Baraza la Rais la Serikali ya Mpito ya Amani," likiongozwa na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo huku Abdelaziz al-Hilu akiwa naibu wake.

RSF inadhibiti sehemu kubwa ya magharibi mwa Sudan, ikiwemo eneo kubwa la Darfur na maeneo mengine kadhaa, lakini inasukumwa nyuma kutoka Sudan ya kati na jeshi, ambalo hivi karibuni limechukua tena udhibiti wa mji mkuu, Khartoum.

RSF na washirika wake walikuwa wamesaini katiba ya mpito mwezi Machi. Jeshi, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, lililaani mipango ya RSF ya kuunda serikali sambamba na kuapa kuendelea kupigana hadi litakapodhibiti maeneo yote ya Sudan — nchi ambayo kwa muda mrefu imekumbwa na migogoro.

Mapambano ya madaraka

Mwezi Februari, RSF na viongozi waasi washirika walikubaliana kuunda serikali kwa ajili ya "Sudan Mpya," wakilenga kupinga uhalali wa utawala unaoongozwa na jeshi.

Dagalo hapo awali alishirikiana madaraka na Burhan kufuatia kuondolewa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir mwaka 2019. Hata hivyo, mapinduzi ya mwaka 2021 yaliyofanywa na vikosi hivyo viwili yaliwaondoa wanasiasa wa kiraia, na kusababisha mvutano wa madaraka kuhusu ujumuishaji wa vikosi wakati wa mpango wa mpito kuelekea demokrasia.

Mgogoro unaoendelea umeharibu Sudan, na kusababisha mgogoro wa kibinadamu "usio na kifani," huku nusu ya idadi ya watu wakikabiliwa na njaa na ukame mkubwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#