Sport
Dollar
40,5860
-0.48 %Euro
47,7946
-0.42 %Gram Gold
4.353,4200
-1.37 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Tume hiyo imetangaza ratiba kamili ya uteuzi, kampeni na upigaji kura kwa ngazi zote husika Tanzania Bara na Zanzibar
Oktoba 29, siku ya Jumatano imetangazwa rasmi siku ya upigaji kura katika tangazo lililotolewa kwa taifa nzima na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jumamosi 26.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambelege alitangaza kuwa kuanzia Agosti 9 hadi 27 Agosti 2025, shughuli ya utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea Urais na Makamu wa Rais. Uteuzi wa wagombea viti hivi utafanyika 27 Agosti 2025.
Shughuli ya utoaji wa fomu za uteuzi kwa wanaowania ubunge na udiwani itafanyika kuanzia 14 Agosti hadi 27 Agosti 2025. Uteuzi rasmi utafanyika 27 Agosti 2025.
Kipindi cha Kampeni - Tanzania Bara
Jajji Mwambelege ametangaza pia kuwa 28 Agosti - 28 Oktoba 2025, kuwa kipindi rasmi cha kampeni za uchaguzi wa Tanzania Bara.
Kampeni za uchaguzi wa Zanzibar utamalizika siku moja kabla, ikiwa ni tarehe 27 Oktoba 2025 ili kuruhusu kufanyika uchaguzi wa mapema.
Uchaguzi huu unafanyika wakati kuna wasiwasi wa ukandamizaji wa upinzani, huku kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha Upinzani CHADEMA Tundu Lissu akiwa anazuiliwa kwa mashtaka mbali mbali ikiwemo uhaini.
Pia chama chake kimefungiwa nje ya shughuli ya uchaguzi 2025 kutokana na kutosajili ndani ya muda uliotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi mapema mwezi Aprili.
Upande wa Chama kinachotawala CCM, Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan anaingia katika uchaguzi wake wa kwanza kama Rais, kwani anamalizia hatamu ya Rais aliyemtangulia John Pombe Magufuli, aliyefariki mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kwa awamu yake ya pili.
Comments
No comments Yet
Comment