Kupitia ukurasa wake wa X, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kuwa, shirika hilo linaendelea kuzisaidia nchi hizo, kukabiliana na kusambaa wa maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeyaomba mataifa mbalimbali duniani, kutoziwekea vizuizi vya usafiri na kibiashara Kenya, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia taarifa za kifo kilichotokana na maradhi ya Ebola, kilichotokea Kenya, siku ya Jumanne.
Kupitia ukurasa wake wa X, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kuwa, shirika hilo linaendelea kuzisaidia nchi hizo tatu, katika kukabiliana na kusambaa wa maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
"Tunatoa wito wa kuondoa vikwazo vyovyote dhidi ya mataifa haya, tunapoendelea kufuatilia hali ya maambukizi katika nchi hizo,” alisema Ghebreyesus.
Kulingana na Mkurugenzi huyo, Kenya iliripoti taarifa za mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola, ambaye ni Mkenya aliyekuwa akiishi DRC.
Aliongeza kuwa, mtu huyo aliugua akiwa DRC, kabla ya kupokea matibabu, na kisha kusafiri kuelekea Nairobi, kupitia Kampala, Uganda.
Mgonjwa huyo, alifariki dunia siku ya Jumatatu, kulingana na Ghebreyesus.
