Sport
Dollar
40,5731
0.03 %Euro
46,9016
-0.34 %Gram Gold
4.340,5600
0.41 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Stephen Abdulkareem Munyakho, alinusurika kunyongwa baada ya kukaa jela miaka 14 Saudi Arabia kwa kosa la mauaji.
Mkenya Stephen Abdulkareem Munyakho, ambaye amekuwa gerezani nchini Saudi Arabia kwa takriban miaka 14 amerudi nyumbani, baada ya kunusurika kuuawa kwa kosa la mauaji.
Munyakho alishutumiwa kumuua mfanyakazi mwenzake raia wa Yemen kwa kumchoma kwa kisu cha kufungua barua, baada ya ugomvi ofisini.
Awali mahakama ilimkuta na hatia ya mauaji bila kukusudia, kutokana na kuwa mfanyakazi mwenzake alimshambulia wa kwanza.
hata hivyo familia ya jamaa huyo kutoka Yemen ilikata rufaa ambapo mahakama ilibaatilisha hukumu ya awali na kumuwekea hatia ya mauaji.
Malipo ya Diyya - ‘Pesa ya damu’
Awali kunyongwa kwake kuliratibiwa Mei 2024 lakini kuakhirishwa mara mbili kufuatia uingiliaji kati wa kidiplomasia wa serikali ya Kenya.
Saudi Arabia inayotumia sheria ya Kiislamu, inaruhusu mshutumiwa wa mauaji kuachiliwa huru iwapo familia ya muathiriwa itakubali kupokea malipo ya damu, inayojulikana kama ‘Diyya’.
Kuachiliwa kwa Munyakho kuliwezekana baada ya familia ya marehemu kukubali diyya ya takriban Sh129 milioni, na kuahirisha hukumu ya kifo iliyotolewa 2024.
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Masuala ya Kigeni na Diaspora, Waziri Mkuu Musalia Mudavadi alitoa shukrani kwa wote walioshiriki katika kupata uhuru wa Munyakho.
Comments
No comments Yet
Comment