Dollar

40,5832

0.01 %

Euro

46,9247

0.08 %

Gram Gold

4.338,7300

-0.03 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa wito wa kutatuliwa kwa changamoto za uwekezaji kati ya bara la Afrika na visiwa vya Karibi.

Majaliwa atoa wito wa kutatua changamoto za uwekezaji Afrika na Karibi

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye anahudhuria Jukwaa la Nne la Biashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibi (ACTIF) alisema kuna umuhimu wa wadau kuja na mbinu za kutatua changamoto zao wenyewe ili kuimarisha uwekezaji.

Majaliwa anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mjini St. George’s, nchini Grenada.

Amesema kuwa changamoto hizo zinapaswa kujadiliwa kwa uwazi na kutaja vikwazo vinavyosababisha kutofanyika kwa biashara kati ya mataifa hayo.

“Mbali ya kujadili changamoto hizo, nchi zetu zinapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye mataifa yetu. Kwetu sisi Tanzania, Aliko Dangote ni mfano hai, amewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ujenzi wa kiwanda cha saruji.” Alisema Kassim Majaliwa.

Ameyasema hayo siku ya Jumatatu wakati akishiriki mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Nne la Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibi (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum-ACTIF 2025).

Viongozi wengine walioshiriki mjadala huo ni Waziri Mkuu wa Dominica, Roosevelt Skerritt; Waziri Mkuu wa Barbados, Mia Amor Mottley; Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda, Gaston A. Browne; Waziri Mkuu wa Saint Kitts na Nevis, Dkt. Terrance Drew; Waziri Mkuu wa St. Lucia, Philip J. Pierre pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#