Dollar

40,5830

0.01 %

Euro

46,9242

0.06 %

Gram Gold

4.338,9400

-0.03 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kituo cha Michezo cha Zaria Courts mjini Kigali kitajumuisha maeneo ya viwanja vya mpira wa vikapu, vifaa vya mafunzo ya michezo, maeneo ya kuuza bidhaa na maeneo ya kuonyesha mitindo ya maisha.

Rwanda yawekeza dola milioni 25 katika uwanja mpya wa mpira wa vikapu

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema Rwanda inajitolea kutumia nguvu za kiuchumi na kijamii kuleta maendeleo katika michezo.

Rwanda imewekeza tena katika michezo kwa kuvumbua kituo kipya cha michezo ndani ya mji mkuu Kigali chenye thamani ya dola milioni 25.

Kitajumuisha maeneo ya viwanja vya mpira wa vikapu, vifaa vya mafunzo ya michezo, maeneo ya kuuza bidhaa na maeneo ya kuonyesha mitindo ya maisha.

“Sikuwa mwanamichezo, angalau sikucheza michezo lakini mimi ni mwanamichezo moyoni. Yote haya hujenga jamii, hujenga familia, hujenga watu binafsi. Ndio jinsi wazo la kujenga jiji hili la michezo liliivyoibuka,” Rais Kagame alisema.

Aliungana na Masai Ujiri, mwanzilishi mwenza wa Giants of Africa, na Andrew Feinstein, Mkurugenzi Mkuu wa Zaria Group, Rais Kagame alizindua vifaa vipya vya Uwanja wa Zaria akikielezea kama kitovu chenye madhumuni mengi cha mijini kinachojumuisha michezo, jamii, burudani na utamaduni.

Serikali inasema kituo hicho cha michezo kimeundwa ili kukuza vipaji vya ndani, kuvutia ushirikiano wa kimataifa, na kuchochea kubuni kazi.

“Na hatukomi hapa. Tunaendelea kukua. Tunaendelea. Takwimu zinaonyesha kuwa kote barani Afrika, kile ambacho michezo inaweza kuleta barani humo kinafikia makumi ya mabilioni. Tunachofanya kama viongozi katika ngazi tofauti ni kuhimiza watu kuwa sehemu ya kutambua wazo hilo na kujipatia faida,” Kagame aliongezea.

Uwekezaji kwa michezo

Rwanda inatambulika kwa kuwekeza vikubwa katika michezo na utalii wa michezo.

Unapozungumzia, kwa mfano, uwanja, watu wanaliona hilo na kuhesabu na kujua kuwa limeajiri wengi, limeleta mengi sana. Na mwingiliano huo karibu na watu hapa na kwengineko, na ulimwengu wote, unazungumza juu ya thamani ya uwekezaji huu,” Rais Kagame alisema.

“Na pia tunajua kuwa takwimu zinaonyesha hata barani Afrika, kwa upande wa michezo, inaingia kwenye mabilioni ukiangalia hela ambazo michezo inaweza kuleta barani, makumi ya mabilioni,” ameongezea.

Kagame amesisitiza umuhimu wa kuwahusisha vijana wa Afrika katika ustawi wa bara hilo, akiwataka kujiamini na kuchangamkia fursa zilizopo.

"Vijana ndio rasilimali ya kwanza ya bara; kila kitu kingine kinakuja baadaye. Lakini lazima waamini katika hilo, waone, na wafanye kazi kwa bidii kuchangamkia fursa zinazopatikana katika bara zima.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#