Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, siku ya Jumatatu aliitisha kikao cha dharura cha Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) ili kupinga hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia.
Akizungumza wakati wa mkutano wa mawaziri wa baraza hilo uliofanyika kwa njia ya mtandao, Abdelatty aliielezea hatua hiyo ya Israel kuwa ni “ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na Hati ya Kisheria ya Kuanzishwa Rasmia kwa Umoja wa Afrika.”
Alionya kuwa kutambuliwa kwa Somaliland na Israel kunadhoofisha misingi ya amani na usalama wa kikanda na kimataifa, hasa katika eneo la Pembe ya Afrika.
Abdelatty alitoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Amani na Usalama la AU ili kujadili suala hilo na kuthibitisha tena umoja na uhuru wa mipaka wa Somalia, pamoja na kukataa hatua za upande mmoja zinazotishia amani na usalama wa kikanda na kimataifa.
Suala la Somalia lawekwa mbele ya Baraza la UN
Jumapili, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) iliitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua msimamo mkali kuhusu hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland. Katika taarifa iliyotolewa kufuatia mkutano wa dharura uliofanyika Cairo, Jumuiya hiyo ilisisitiza haki ya Mogadishu ya kujilinda kisheria katika kulinda eneo lake.
Israel ikawa nchi ya kwanza duniani kuitambua Somaliland kama taifa huru siku ya Ijumaa, hatua iliyokosolewa vikali na Uturuki, mshirika wa karibu wa Somalia, pamoja na nchi nyingine za Afrika na Mashariki ya Kati.
Upinzani wa kimataifa dhidi ya hatua hiyo uliendelea kuongezeka, huku nchi nyingi zikiilaumu kama ukiukwaji wa sheria za kimataifa na tishio kwa uthabiti wa kikanda.
Siku ya Ijumaa, Somalia ilisisitiza tena dhamira yake isiyoyumba kuhusu mamlaka yake, umoja wa kitaifa, na uhuru wa mipaka yake kufuatia hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland.
Sehemu ya Somalia
Somaliland, iliyoko kaskazini mwa Somalia, haijawahi kupata utambuzi rasmi tangu ilipotangaza kujitenga na Somalia mwaka 1991.
Somalia inaichukulia Somaliland kuwa sehemu ya eneo lake, na inaona mikataba au ushirikiano wowote wa moja kwa moja nayo kuwa ni ukiukwaji wa uhuru na umoja wa nchi hiyo.
Comments
No comments Yet
Comment