Dollar

42,9363

0.07 %

Euro

50,6390

0.14 %

Gram Gold

6.164,2700

-1.38 %

Quarter Gold

10.214,5800

-1.21 %

Silver

103,3600

-4.49 %

Uingereza imeweka vizuizi vya viza kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na "ushirikiano mdogo" wa nchi hiyo katika kuwarudisha wahamiaji haramu, serikali ya Uingereza ilisema.

Uingereza yabana utoaji viza kwa raia wa DRC kwa kukataa kuwapokea wahamiaji waliorejeshwa

Uingereza imeweka vikwazo vya viza kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na "ushirikiano mdogo" kuhusu kurejesha wahamiaji haramu, ilisema serikali ya Uingereza.

Hatua zaidi, hata kusitisha kabisa utoaji wa viza, zitatumika ikiwa ushirikiano hautaimarika "haraka", ilisema wizara ya mambo ya ndani katika taarifa mwishoni mwa Jumamosi.

Vikwazo hivyo vina maana kwamba viongozi wa hadhi ya juu na watunga sera wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakosa huduma za upendeleo za viza, wakati mchakato wa utoaji wa viza kwa njia ya haraka umefutwa kwa raia wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Haya yalitangazwa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Shabana Mahmood, mwezi Novemba kuwatishia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na Namibia marufuku za viza hadi pale watakapokubali kupokea wahamiaji wasiokuwa wa kawaida.

Angola, Namibia wakubaliana kupokea wahamiaji wanaorudishwa

Wizara ya mambo ya ndani ilisema nchi hizo tatu za Afrika zimekuwa "zikizuia mara kwa mara" juhudi za kuondoa maelfu ya wahamiaji haramu.

Uingereza ilishtumu nchi hizo kwa kukataa kupokea raia wao na badala yake kuwataka kila mmoja asaini nyaraka zao wenyewe, jambo ambalo kisheria liliwapa uwezo wa kuzuia kuhamishwa wao.

Hata hivyo, Angola na Namibia zilikubali 'kuimarisha taratibu zao' na kukubali kurudisha 'wahamiaji haramu', hivyo mataifa hayo hayatakabiliwa na vikwazo hivyo, ilisema wizara ya mambo ya ndani.

Kulikuwa na mawasiliano ya hivi karibuni na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini Mahmood alionya kwamba taifa hilo la Afrika ya Kati linatakiwa "kufuata sheria."

Sheria kali za kuomba hifadhi

"Kama mmoja wa raia wao hana haki ya kuwa hapa, wanatakiwa wampokee," alisema.

"Nawashukuru Angola na Namibia na napongeza ushirikiano wao. Sasa ni wakati wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya jambo sahihi. Chukuwa raia wako au upoteze fursa ya kuingia nchini mwetu."

Hatua hizi za viza zilitolewa kama sehemu ya mabadiliko ambayo Mahmood alitangaza mwezi Novemba akitaka kuwepo kwa sheria kali za kuomba hifadhi nchini Uingereza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#