Sport
Dollar
42,9693
0.04 %Euro
50,7212
0.14 %Gram Gold
6.030,6700
0.79 %Quarter Gold
10.064,2000
0 %Silver
102,9900
2.4 %Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, atafanya ziara rasmi nchini Uturuki siku ya Jumanne, kwa mwaliko wa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumanne na mkurugenzi wa mawasiliano wa nchi hiyo.
Katika ziara hiyo Rais wa Uturuki na mwenzaka wa Somalia wanatarajiwa kujadili masuala kadhaa ikiwemo kutathminiwa kwa kina nyanja zote za ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
“Wakati wa mkutano huo, uhusiano wa mataifa mawili kati ya Uturuki na Somalia utatathminiwa kwa kina katika nyanja zote, na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuimarisha zaidi ushirikiano zitajadiliwa,” alisema Burhanettin Duran kupitia ukarasa wa mtandao wa kijamii wa Uturuki, NSosyal.
Mikutano hiyo pia itashughulikia maendeleo ya hivi karibuni katika mapambano ya Somalia dhidi ya ugaidi na juhudi za Serikali ya Somalia kuhakikisha umoja wa kitaifa, pamoja na masuala ya maendeleo ya kikanda.
Comments
No comments Yet
Comment