Dollar

42,9442

0.02 %

Euro

50,6653

-0.04 %

Gram Gold

5.983,1700

-0.01 %

Quarter Gold

10.064,2000

0 %

Silver

99,7100

-0.86 %

Afrika Kusini imeonya kwamba uamuzi wa Israel wa kutambua eneo la Somaliland kama taifa huru ni “tishio la moja kwa moja” dhidi ya amani katika Pembe ya Afrika.

Afrika Kusini yalaani hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland kama taifa huru

Afrika Kusini kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ilisema kuwa utambuzi huo unakiuka uhuru na mipaka ya Somalia.

“Kitendo cha Israel kinachochea mgawanyiko na kinaweza kusababisha hali ya kutokuwa na utulivu,” taarifa ya wizara hiyo ilisisitiza.

Wizara hiyo ilibainisha kuwa kuna tofauti dhahiri kati ya kuondoa ukoloni na kujitenga, na kusema: “Kuondoa ukuloni ni kurejesha uhuru; na kujitenga ni kuharibu uhuru.”

Israel yalaaniwa kimataifa

Afrika Kusini ilisema inaunga mkono kanuni ya Umoja wa Afrika ya “uti possidetis”, inayozingatia kuheshimu mipaka iliyopatikana wakati wa uhuru ili kuepuka migogoro, na kuhamasisha jamii ya kimataifa kupinga “uingiliaji wa nje” wa Tel Aviv na kusaidia Somalia iwe na mshikamano na utulivu.

Israel imekuwa nchi ya kwanza duniani kutambua Somaliland kama taifa huru, hatua iliyolaaniwa na Uturuki, ambayo ni mshirika wa karibu wa Somalia, pamoja na nchi nyingine barani Afrika na Mashariki ya Kati.

Mzozo wa kimataifa umeongezeka kutokana na utambuzi wa Israel kwa Somaliland, huku nchi nyingi zikieleza kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na tishio kwa utulivu wa eneo.

Somaliland, iliyoko kaskazini mwa Somalia, haijawahi kutambuliwa rasmi tangu itangaze kujitenga na Somalia mwaka 1991.

Somalia inaona Somaliland kama sehemu muhimu ya taifa lake, na inaona mikataba yoyote ya moja kwa moja au ushirikiano na eneo hilo kama ukiukaji wa uhuru na mshikamano wa nchi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#