Sport
Dollar
40,6704
0.08 %Euro
46,4161
-0.19 %Gram Gold
4.308,4900
0.21 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Waziri wa Sudan ametoa shukrani zake kwa nchi ya Misri kuendelea kwake kuunga mkono uhuru na usalama wa Sudan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty alizungumza kuhusu juhudi za kufikia amani nchini Sudan katika mazungumzo ya simu siku ya Jumatano na mwenzake wa Sudan Omar Siddiq.
Pande hizo mbili ziliangalia upya "juhudi za Misri zinazolenga kufikia amani na utulivu nchini Sudan na kuhifadhi rasilimali za watu wa Sudan, ikiwa ni pamoja na majadiliano ndani ya mfumo wa pande nne husikia za kimataifa zinazojadili kuhusu Sudan, ambayo Misri inashiriki," Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema katika taarifa.
Abdelatty alithibitisha tena kwamba Misri itaendelea kuiunga mkono Sudan katika kulinda uhuru wake, taasisi zake za kitaifa, umoja wa kitaifa na mipaka yake. Alisisitiza pia kuwa Misri inapinga vikali hatua yoyote itakayohatarisha umoja wa Sudan.
Siddiq alielezea shukrani zake kwa "kuendelea kuunga mkono Misri kwa uhuru na usalama wa Sudan" na akaelezea matarajio yake ya "kukuza zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili," taarifa hiyo iliongeza.
Siku ya Jumamosi, muungano wa Sudanese Founding Alliance, unaoongozwa na Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), ulitangaza kuundwa kwa serikali nyengine Sudan inayoongozwa na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo.
RSF na makundi kadhaa washirika walitia saini mkataba nchini Kenya Februari 22 ili kuanzisha serikali sambamba nchini Sudan.
Jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF wamekuwa wakipigana vita tangu Aprili 2023 ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 na wengine milioni 14 kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za mitaa.
Utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani, unakadiria idadi ya vifo kuwa karibu 130,000.
Comments
No comments Yet
Comment