Dollar

42,8363

0.01 %

Euro

50,6653

0.52 %

Gram Gold

6.173,3500

1.04 %

Quarter Gold

9.975,1400

0 %

Silver

95,9200

1.13 %

Mapigano yaliibuka siku ya Jumatatu karibu na mji wa Uvira katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya waasi wa M23 na wapiganaji wanaounga mkono serikali, siku chache baada ya M23 kuahidi kuondoka katika mji huo, vyanzo vya eneo hilo vilisema.

Mapigano yarindima mji wa mpaka wa DRC wa Uvira kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23

Mapigano yaliibuka siku ya Jumatatu karibu na mji wa Uvira katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya waasi wa M23 na wapiganaji wanaounga mkono serikali, siku chache baada ya M23 kuahidi kuondoka katika mji huo, vyanzo vya eneo hilo vilisema.

Waasi wa M23 walidhibiti mji wa kimkakati karibu na mpaka wa Burundi mapema mwezi huu, muda mfupi baada ya serikali za DRC na Rwanda kutia saini makubaliano ya amani jijini Washington ambayo Rais wa Marekani Donald Trump aliyataja kuwa "miujiza mikubwa."

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ameshtumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya amani waliyotia saini na jirani zake Disemba 4, na kuapa kuchukuwa "hatua" ya kujibu. Hata hivyo, Rwanda, inakanusha, na badala yake inadai jirani zake, DRC na Burundi, wanakiuka makubaliano ya kusitishwa mapigano.

Kiongozi wa kisiasa wa M23, Corneille Nangaa, alitangaza kuwa kundi hilo "litaondoa vikosi vyake kutoka mji wa Uvira, kama walivyotakiwa kufanya hivyo na wapatanishi wa Marekani."

Makabiliano ya risasi

Hata hivyo, wanachama askari kanzu wa M23 walibaki katika mji huo, kulingana na vyanzo eneo hilo na vya usalama.

M23 na vikosi vinavyounga mkono serikali vinavyojulikana kama Wazalendo walifyatuliana risasi siku ya Jumatatu "ambazo zilisikika kote Uvira", Mafikiri Mashimango, kiongozi wa eneo hilo wa asasi isiyokuwa ya serikali, aliiambia AFP.

Watu hawakutoka nje kwa ajili ya usalama wao na shughuli "zilisimama" katika mji huo, kulingana na mkazi aliyewasiliana kwa njia ya simu.

Mapigano yanaonekana kuendelea katika milima iliyozunguka na maeneo ya kusini na kusini magharibi ya mji, ikiwemo karibu na mji wa bandari wa Kalundu katika Ziwa Tanganyika, wakazi walisema.

'Mapinduzi ya vyombo vya habari'

Bomu moja lilianguka eneo la Mulongwe, kusini mashariki mwa Uvira, "na risasi ziliskika juu ya nyumba", alisema mkazi mmoja.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeiita ahadi ya M23 kuondoka "mapinduzi ya vyombo vya habari kutaka kuhadaa watu" na kushtumu kundi hilo kwa kupeleka wapiganaji tena katika milima ya Uvira.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#