Sport
Dollar
42,8152
0.02 %Euro
50,2918
0.26 %Gram Gold
6.068,6600
1.61 %Quarter Gold
9.962,2400
0.99 %Silver
95,2000
2.9 %Kwa wiki kadhaa sasa maeneo mengi ya Mkoa wa Dar es Salaam yamekuwa yakikabiliwa na uhaba wa maji hatua inayowalazimu kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa mpango wa uchimbaji wa visima 14 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua ya kuongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi kufuatia agizo la Waziri wa Maji wa Tanzania, Jumaa Aweso.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya uchimbaji wa visima katika Jimbo la Kivule, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema kuwa kati ya visima hivyo, vitano vitachimbwa katika Jimbo la Ilala huku visima tisa vikichimbwa katika Jimbo la Kivule kwa lengo la kuhudumia wananchi wengi zaidi.
Mhandisi Bwire ameeleza kuwa katika Jimbo la Kivule, visima vitachimbwa katika maeneo ya Kivule, Magole A, Kerezange, Bombambili pamoja na Msongola Mtaa wa Kidole.
Ameongeza kuwa DAWASA pia imechukua hatua za kufufua visima vilivyokuwepo katika maeneo ya Mwananyamala, Tandale na Mburahati, ambapo kwa sasa visima 14 tayari vinatoa huduma kikamilifu kwa wananchi.
Comments
No comments Yet
Comment