Sport
Dollar
42,8204
0.03 %Euro
50,4063
0.48 %Gram Gold
6.103,6100
2.2 %Quarter Gold
9.975,1400
1.12 %Silver
94,2700
1.9 %Ushirikiano kati ya Uturuki na mataifa ya Afrika umeimarika sana katika miaka ya hivi karibuni, katika sekta mbalimbali ikiwemo ulinzi.
Uturuki imeahidi kuendelea kushirikiana na mataifa ya Afrika ikiwemo katika mafunzo na usaidizi wa kiufundi, kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na kuimarisha usalama katika bara hilo.
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Yaşar Güler, ameeleza wakati wa mkutano na wawakilishi wa mashirika ya habari jijini Ankara mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kufanyia tathmini shughuli za wizara yake.
"Kuhusu Afrika, kuimarisha ushirikiano wetu katika masuala ya ulinzi na mataifa ya Afrika – ambayo tuna uhusiano wa kihsitoria nao pamoja na kitamaduni – na kwa hivyo kuchangia katika usalama na uthabiti wa bara hilo kunabaki kuwa miongoni mwa vipaumbele vyetu," Güler alisema.
"Kulingana na maombi tuliyoyapokea, tunaendelea kutoa mafunzo, fedha, vifaa, na kuwaunga mkono kiufundi Majeshi ya mataifa ya Afrika, hivyo kuchangia katika juhudi za kuimarisha uwezo wao. Kwa muktadha huu ushirikiano wetu wa mafunzo ya kijeshi, tunatoa mafunzo ya lugha ya Kituruki kwa nchi 12 (Somalia, Libya, Senegal, Gambia, Burkina Faso, Cameroon, Mali, Djibouti, Nigeria, Niger, Gabon, na Guinea) kupitia wizara yetu, Wakf wa Uturuki wa Maarif, na Taasisi ya Yunus Emre."
‘Libya yenye Umoja’
Katika juhudi za Uturuki kwa ajili ya kuwa na Libya yenye umoja, waziri alisisitiza "Uhusiano wa kihistoria wa siku nyingi" kati ya nchi hizo mbili, akiieleza Libya kama "jirani zetu wa Mediterani", na kuhakikisha dhamira ya Uturuki kwa amani.
"Mafunzo yetu ya kijeshi, usaidizi, ushirikiano, na shughuli za ushauri nchini Libya zinaendelea kwa lengo la kuwa na Libya moja kumehakikisha kuwepo kwa uhuru wake na umoja wa kisiasa, kuishi kwa amani, utulivu, na uthabiti," Yaşar Güler aliongeza.
"Ushirikiano wetu wa masuala ya baharini, ni msingi ambao uliwekwa kwenye makubaliano kuhusu shughuli za maeneo ya bahari yaliyotiwa saini 2019, yameimarishwa na kujumuisha sekta kama ulinzi wa nishati na kukabiliana dhidi ya uhamiaji haramu," alieleza.

"Hatua zinapigwa kuelekea lengo la kuwa na 'Libya yenye Umoja', matokeo ya juhudi zetu na majadiliano ambayo tumeendeleza na pande zote katika sera ya msingi. Kwa muktadha huu, tunaendelea kuunga mkono kwa dhati mchakato wa kisiasa unaoongozwa na Umoja wa Mataifa."
Somalia ni mshirikika mwingine muhimu wa Uturuki barani Afrika, ambapo Yaşar Güler alisisitiza kuwa mchango wa Uturuki katika maeneo mbalimbali unaendelea kuongezeka.
‘Heshima na kuaminiana’
"Mafunzo yetu, kushauriana, na kuunga mkono shughuli zenye lengo la kuhakikisha usalama na uthabiti katika taifa rafiki la Somalia yanaendelea kuongezeka. Zaidi ya hayo, hivi karibuni tumeanzisha Kikosikazi cha Angani nchini Somalia, kinachojumuisha helikopta za mashambulizi," alisema.
Waziri pua alieleza kuongezeka kuimarika kwa ushirikiano wa masuala ya bahari kati ya Uturuki na Senegal.
"Ndege zetu za doria ya baharini zilizoko Senegal zimeanza shughuli zake mwezi Oktoba kusaidia katika utafutaji na uokoaji pamoja na tathmini na mafunzo ya tathmini ya baharini na kusaidia Majeshi ya Senegal. Vile vile, tunaendelea kuunga mkono mafunzo kwa majeshi ya Mali na Niger," Güler alisema.
"Ningependa kusisitiza kuwa tunaweka umuhimu mkubwa kwa suala la usalama na uthabiti barani Afrika, na tunaimarisha uhusiano wetu na marafiki zetu barani Afrika kila siku, kwa misingi ya heshima na kuaminiana," aliongeza.
Comments
No comments Yet
Comment