Dollar

42,8215

0.01 %

Euro

50,5418

0.21 %

Gram Gold

6.111,8500

0.03 %

Quarter Gold

9.975,1400

0 %

Silver

95,0400

0.2 %

Somalia, Uturuki waimarisha uhusiano katika sekta ya uvuvi kwa kutia saini makubaliano mapya

Waziri wa uvuvi wa Somalia apongeza ushirikiano wa kimkakati na Uturuki
  • Kampuni ya pamoja ya Uturuki na Somalia itasimamia shughuli za uvuvi, utoaji leseni chini ya ushirikiano wa kitaasisi

  • Makubaliano hayo 'ni ya mfumo wa faida kwa nchi zote mbili,' anasema Ahmed Hassan Aden

ISTANBUL

Waziri wa uvuvi wa Somalia siku ya Jumatatu alipongeza makubaliano yaliyotiwa saini ya “Ushirikiano wa Kimkakati na Huduma” na Uturuki, akisema utachangia katika uchumi wa Somalia na kusaidia kuanzisha mfumo wa ushirikiano wa uchumi wa kitaasisi kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na Anadolu, Waziri wa Uvuvi wa Somalia Ahmed Hassan Aden alisisitiza kuwa makubaliano yaliyotiwa saini na taasisi kubwa ya Uturuki ya OYAK, ni muhimu sana kwa pande zote mbili katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa nchi hizo.

Alisema ushirikiano katika sekta ya uvuvi utatekelezwa kupitia kampuni ya pamoja ya SOMTURK, akiongeza kuwa wote watu wa Somalia na Uturuki watafaidika kutoka kwa ubia huo.

“Mkataba huo unatoa fursa kwa mfumo wa ushirikiano wenye faida kwa nchi zote mbili,” Aden alisema.

Usalama baharini, kupambana dhidi ya uvuvi haramu

Aden alisema kuwa makubaliano hayo pia yanajumuisha suala la kulinda raslimali zilizoko kwenye bahari ya Somalia kwa ushirikiano na Uturuki.

“Ushirikiano huu utachangia usalama wa baharini kwa Somalia wakati ukihakikisha ulinzi endelevu wa raslimali za baharini,” alisema.

Aliongeza kuwa kukabiliana na uvuvi haramu, ambao haufahamiki na hauratibiwi katika Bahari Hindi, hasa katika pwani ya Somalia, ni miongoni mwa malengo muhimu ya mkataba huo.

Waziri huyo wa Somalia alisema makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ufuatiliaji wa masuala ya baharini wa Somalia na uwezo wa utekelezaji katika maeneo yake ya bahari, pamoja na kuimarisha uwezo wa nchi hiyo kulinda mipaka yake ya bahari, haki za umiliki na fursa za kiuchumi katika Bahari Hindi.

Kampuni ya SOMTURK, mfumo wa leseni

Aden alisema kuwa kampuni ya SOMTURK, iliyoanzishwa kwa ushirikiano wa Uturuki na Somalia, itaratibu shughuli zote za kutoa leseni za uvuvi.

Alieleza kuwa mamlaka hiyo ya kudhibiti, mchakato wa leseni na kuidhinisha inabaki kuwa na Wizara ya Uvuvi.

“Mfumo huu utaimarisha uwezo wa taasisi nchini wakati ukiwa na jukumu la kuratibu kimataifa,” alisema, akiongeza kuwa maombi ya leseni kutoka kampuni za kimataifa na za nyumbani pia yatahsughulikiwa kwa mfumo huo.

Mafanikio ya ajira na uchumi kwa watu wa Somalia

Akisisitiza kuhusu makubaliano hayo kuwa yanawakilisha ushirikiano wa kimkakati, Aden aslisema yatafunguwa fursa zingine mustakabali wa uchumi kati ya nchi hizo mbili.

“Kwa kugawanya mapato kupitia kampuni ya SOMTURK, faida za makubaliano haya itaonekana kwa wote watu wa Somalia na Uturuki, kutoa fursa kwa nchi zote kufaidika kiuchumi,” alisema.

Aliongeza kuwa makubaliano yatatoa fursa ya ajira kwa watu wa Somalia, akisisitiza ni faida ya moja kwa moja kwa watu wa eneo hilo.

Kulingana na Aden, ushirikiano huo utachangia maendeleo ya bandari, na miundombinu ya barafu ya kuhifadhi bidhaa, pamoja na majengo katika sekta ya uvuvi ya Somalia.

“These developments will generate new job opportunities for young people, provide vocational training and support the expansion of foreign trade,” he said.

Sekta ya Uturuki ya uvuvi, ushirikiano

Aden alieleza kuwa Somalia ina uwezo mkubwa wa uvuvi katika ukanda wake wa pwani ambao haujatumika vizuri.

“Kutoa nafasi kwa sekta ya uvuvi ya Uturuki kufikia bandari za Somalia, bahari yake kutatoa fursa kwa meli za Uturuki kufanya shughuli za uvuvi katika maeneo haya,” alisema.

Alisisitiza kuwa Somalia pia itafaidika na utajiri wake wa asili kutoka kwa kampuni za Uturuki, kuimarisha mitazamo ya kiuchumi na kimkakati ya ushirikiano wa nchi zote mbili.

Alisema makubaliano hayo yatathibitisha ukuaji wa ushirikiano wa mataifa hayo mawili ambao umekuwa ukiimarika katika miaka ya hivi karibuni.

Makubaliano yaliyotiwa saini Disemba 17

Mkataba wa uvuvi ulitiwa saini Disemba 17 kati ya Wizara ya Uvuvi ya Somalia na OYAK.

Chini ya makubaliano hayo, SOMTURK ilianzisha nchini Somalia kusaidia wizara kuratibu shughuli zote za leseni kuhusu uvuvi katika eneo maalum la kiuchumi la Somalia.

Zaidi ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kiufundi kati ya nchi hizi mbili, makubaliano hayo yanatarajiwa kutengeneza mfumo endelevu wa mapato, kuongeza ajira kupitia kuchakata samaki, kuimarisha uchumi wa eneo hilo, na kuhakikisha kuwa unachangia katika maslahi ya watu wa Somalia.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#