Maelfu ya Walibya walijitokeza kwa ajili ya mazishi ya mtoto wa Gaddafi ambaye alipigwa risasi na kuuawa wiki hii.

Maelfu ya Walibya wajitokeza kumzika mtoto wa Gaddafi

Maelfu ya watu walimiminika siku ya Ijumaa katika kaskazini-magharibi mwa Libya kuhudhuria mazishi ya Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi. Saif al-Islam aliuawa mapema wiki hii baada ya watu wanne waliokuwa wamevaa barakoa kuvamia nyumba yake na kumpiga risasi hadi kufa.

Waombolezaji walibeba jeneza lake katika mji wa Bani Walid, uliopo kilomita 146 (maili 91) kusini-mashariki mwa mji mkuu, Tripoli, pamoja na picha kubwa za Saif al-Islam—ambaye mara nyingi alijulikana kwa jina lake la kwanza—na baba yake.

Muammar Gaddafi aliitawala Libya kwa zaidi ya miaka 40 kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 2011. Aliuawa baadaye mwaka huo katika mji wake wa Sirte, wakati mapigano nchini Libya yalipozidi na kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.

Msafara wa mazishi ulipoanza na umati wa watu kuongezeka, kundi dogo la wafuasi wake lilichukua jeneza la Saif al-Islam na baadaye kumswaliya na kumzika.

Aliuawa kwa kupigwa risasi

Saif al-Islam, mwenye umri wa miaka 53, aliuawa siku ya Jumanne ndani ya nyumba yake katika mji wa Zintan, uliopo kilomita 136 (maili 85) kusini-magharibi mwa Tripoli, kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Libya.

Mamlaka zilisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa alipigwa risasi hadi kufa, lakini hazikutoa maelezo zaidi.

Wanachama wa kisiasa ya Saif al-Islam baadaye walitoa taarifa kuwa “watu wanne waliovaa barakoa” waliivamia nyumba yake na kumuua, wakiyataja kuwa “mauaji ya kikatili na ya hila,” baada ya kuzima kamera za usalama.

“Maumivu ya kumpoteza yananilemea sana moyoni, na yanaongezeka zaidi kwa sababu siwezi kumuaga nikiwa ndani ya nchi yangu — maumivu ambayo maneno hayawezi kuyapunguza,” aliandika kaka yake Saif al-Islam, Mohamed Gaddafi, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook siku ya Ijumaa.

“Lakini faraja yangu ni kwamba wanaanchi waaminifu wa taifa wanatimiza wajibu wao na watampa buriani inayostahili hadhi yake,” aliandika kaka huyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#