Dollar

43,5178

0.07 %

Euro

51,5292

0.16 %

Gram Gold

7.122,6900

3.09 %

Quarter Gold

12.083,1300

0 %

Silver

126,6200

6.55 %

Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya kikao kilichofanyika Doha, kilichohusisha wawakilishi wa kikosi cha waasi cha M23 na wajumbe kutoka DRC.

Ujumbe wa UN kuwasili DRC kusaidia jitihada za kusitisha mapigano

Umoja wa Mataifa unatarajiwa kutuma ujumbe wake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanikisha usitishwaji wa mapigano.

Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya kikao kilichofanyika Doha, kilichohusisha wawakilishi wa kikosi cha waasi cha M23 na wajumbe kutoka DRC.

“Wakati wa kikao hicho, pande zote mbili zilikubaliana kuwepo na mfumo maalumu wa ufatiliaji wa kukomesha mapigano”, ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na serikali ya Qatar.

Mwezi Januari mwaka jana, kikundi cha M23 kilidhibiti mji wa Goma, kabla ya kushikilia mji wa Bukavu, mwezi uliofuata.

Kwa miezi kadhaa sasa, Qatar imekuwa msuluhishi kati ya DRC na kikundi cha waasi cha M23.

Makubaliano ya kumaliza mapigano yalifikiwa mwezi Julai mwaka 2025.

Mwezi Disemba mwaka jana, mkataba mwingine ulisainiwa kati ya DRC na Rwanda.

Licha ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, mapigano yameendelea kushuhudiwa katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#