Tume ya Umoja wa Afrika imeliita shambulio la hivi karibuni katika uwanja mmoja wa ndege nchini DRC , kama “tukio la kigaidi”.

AU: Shambulizi la M23 kwenye uwanja wa ndege ni ‘tukio la kigaidi’

Kikundi cha waasi cha M23, kimesema kilihusika la shambulio hilo lililotokea mwishoni mwa juma, katika uwanja wa ndege wa Kisangani.

Kulingana na tume hiyo, shambulio hilo lilihatarisha usalama wa raia na ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za kibinadamu.

"Shambulio hilo ni sawa na kitendo cha kigaidi,” ilisema tume kupitia ukarasa wa X.

Kikundi hicho kimedai kuharibu ndege iliyokuwepo uwanja ni hapo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa utatuma ujumbe maalumu nchini DRC kusaidia mchakato wa usitishwaji mapigano katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#