Ufaransa inadaiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi Burkina Faso.

Urusi yashutumu Ufaransa kwa njama za kuwaondoa viongozi wa Afrika

Idara ya Ujasusi ya Urusi (SVR) imetoa tuhuma nzito dhidi ya Ufaransa, ikisema Rais Emmanuel Macron ameidhinisha oparesheni za kijasusi zinazolenga kuwaondoa au kuwaua viongozi wa Afrika wanaoonekana “wasiotakiwa” na Paris.

Kwa mujibu wa SVR, Ufaransa inajaribu kurejesha ushawishi wake barani Afrika baada ya kupoteza nafasi katika makoloni yake ya zamani, ambako vikosi vya kizalendo vimechukua madaraka na kutanguliza maslahi ya wananchi wao.

Shirika hilo lilidai kuwa Ufaransa ilihusika katika jaribio la mapinduzi Burkina Faso Januari 3, likiwa na mpango wa kumuua Rais Ibrahim Traore. Aidha, SVR imesema juhudi hizo sasa zimeelekezwa Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar, zikilenga kuondoa viongozi kama Assimi Goita na Michael Randrianirina.

SVR pia imetuhumu Ufaransa kushirikiana na makundi ya kigaidi na kupata msaada wa Ukraine kupitia drones na wakufunzi wa kijeshi. Kwa mujibu wa Urusi, hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa kudhoofisha harakati za Pan-Africanism na kuimarisha ushawishi wa kifedha na kisiasa wa Paris.

CHANZO: Newstimehub

#