Akifunga kambi hiyo, Oktoba 9, 2026 Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Malawi, Bestone Chisamile, alisema kuwa hospitali ya Benjamin Mkapa inatekeleza kwa vitendo ushirikiano wa matibabu bingwa.
Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyoko mkoani Dodoma, Tanzania, wamehitimisha rasmi kambi yao ya matibabu nchini Malawi.
Wakati wa kambi hiyo, iliyodumu kwa kipindi cha wiki mbili, madaktari hao walitoa huduma mbalimbali, ikiwemo, upasuaji wa mifupa, upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu, matibabu ya figo na tathmini ya upandikizaji wa figo pamoja na magonjwa ya selimundu.
Mengine, ni magonjwa ya mfumo wa mkojo na kutibu majeraha ya kuungua na moto.
Akifunga kambi hiyo, Oktoba 9, 2026 Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Malawi, Bestone Chisamile, alisema kuwa hospitali ya Benjamin Mkapa inatekeleza kwa vitendo ushirikiano wa matibabu bingwa.
"Ushirikiano wa kiafya kati ya Malawi na Tanzania unatekelezwa kupitia kambi ya matibabu ya kibingwa nchini Malawi. Hata hivyo tumeanza majadiliano, ambayo yataangazia manufaa ya kambi hiyo kwa wagonjwa pamoja na umuhimu wa kurasimisha ushirikiano mpana zaidi unaojumuisha huduma za matibabu, mafunzo ya wataalamu, masuala ya dawa na rufaa za wagonjwa,” alisema Chisamile.
Kwa upande wake, balozi wa Tanzania nchini Malawi, ameielezea kambi hiyo, kama fusra muhimu kwa raia wa Malawi na madaktari wa nchi hiyo.
"Kambi hii imewanufaisha wagonjwa zaidi ya 800, huku baadhi wakipewa rufaa ya hospitali ya Benjamin Mkapa,” alisema.
