Sport
Dollar
41,8596
0.09 %Euro
48,8346
0.41 %Gram Gold
5.660,6900
1.64 %Quarter Gold
9.570,2800
2.24 %Silver
71,3300
3.04 %Ofisi ya Rais aliyeondolwa madarakani wa Madagascar imelaani “hatua haramu” iliyotolewa na kikosi cha kijeshi kuhusu kusimamishwa kutumika kwa katiba.
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Madagascar amesema kupitia shirika la habari la Associated Press akiwa kambini kwake Jumatano kwamba “anachukua nafasi ya urais.”
Kanali Michael Randrianirina, aliyeongoza uasi wa wanajeshi alimuondoa mamlakani Rais Andry Rajoelina, alisema anatarajia kuapishwa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo la Bahari ya Hindi katika siku chache zijazo.
Vile vile alisema anachukua wadhifa wa mkuu wa nchi baada ya Mahakama ya Katiba ya Juu ya nchi hiyo kumwalika kufanya hivyo, kufuatia kutoweka kwa Rajoelina, ambaye alikimbia Madagascar baada ya uasi huo.
Mapema Jumanne, ofisi ya Rais aliyeondolewa Madagascar ililaani kile ilichokiita “hatua haramu” iliyolotolewa na kikosi maalum cha kijeshi cha CAPSAT kuhusu kusitishwa kutumika kwa katiba.
Mapinduzi ya kijeshi
Ofisi ya Rais iliita kikosi cha CAPSAT kama “kundi la waasi wa kijeshi”, na kuongeza ya kwamba uwepo wa jeshi katika ikulu ya rais ni “kitendo cha wazi cha jaribio la mapinduzi na ukiukaji mkubwa wa sheria za Jamhuri.”
“Tendo hilo ni uvunjaji wa wazi wa Katiba, misingi ya demokrasia, na kiapo cha kila mwanajeshi cha kulinda Taifa na taasisi zake halali,” taarifa hiyo ilisema.
Kikosi cha maalum cha kijeshi cha CAPSAT, kilitangaza Jumanne kwamba kimesimamisha kutumika kwa katiba na kumuondoa Rais Andry Rajoelina madarakani kwa kuzingatia hoja ya bunge ya kumwondoa madarakani, pamoja na kuchukua mamlaka, kulingana na mwandishi wa Anadolu.
Comments
No comments Yet
Comment